Wanachapa wapya wakipokea Kadi za CCM
 Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kulia akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi wa kijiji Koma na Kwale kata ya Mwandege.(Picha na Emmanuel Massaka)
 



Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wameombwa  kuweka tofauti zao pembeni na badala yake kukisaidia chama hicho ili kishinde kwa kishindo.

Hayo yamesemwa na mgombea Ubunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega wakati alipokuwa kwenye kampeni katika kijiji cha Mkokozi na Chatembo kata ya Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akiwa katika kata hiyo Ulega amesema serikali ya  chama cha Mapinduzi chini ya Daktari John Pombe Magufuli  imefanya makubwa ndani ya Kata hiyo Kwa miaka mitano kwa upande wa elimu, afya na maji.

Ulega ambaye pia  ni Naibu Waziri wa Mifugo Mifugo Uvuvi ameongeza kuwa ndani ya miaka tano katika Kata hiyo wamejenga shule ya msingi na secondari katika eneo la Kipara Mpakani na wanajenga Shule nyingine ya sekondari katika kijiji cha Chatembo,Lengo kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na watoto kutembea umbali mrefu. 

Sanjari na hayo Ulega hakusita kutoa shukrani kwa wananchi hao kwa namna ambavyo wameunga mkono juhudi za maendeleo kwa miaka mitano, na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono Kwa kuchangia mifuko 400 ya saruji, ambayo 200 Kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na  200 mingine  kwa ajili ya Shule mifuko. 

Mgombea huyo amesema wakati wanaingia madarakani kipindi kilichopita vijiji vilivyokuwa na umeme ni kipara mpakani na mwandege lakini miaka mitano ijayo  vijiji vyote vinaenda kupata umeme.

Aidha Ulega amesema kuwa,ameomba eneo la  msitu wa kipara mpakani kwa ajili ya huduma za kijamii,ambapo kwa sasa kuna shule ya msingi na secondari na panaenda kujengwa kituo cha kisasa cha mabasi kitakacho kwenda kuinua uchumi wa wanamkuranga. 

Hata hivyo mgombea huyo amesema mpaka sasa serikali imeshasajili kilomita 121za barabara tarura,hivyo barabara ya   Mkokozi mpaka Lugwadu na ya Chatembo zita tengenezwa. 

Sambamba na hayo Ulega amesema walishafanya harambee kuhusu kilima cha barabara ya Mkokozi Lugwadu kwa ajili ya matengenezo kwa  kuweka karavati na kufukia mabonde pamoja na kufungua daraja la Mtikatika liweze kupitika wakati wote 

Akihitimisha manzungumzo yake wakati akiendelea na kampeni katika kata ya mwandege, Ulega amesema hatowaacha  nyuma kinamama na kuwaahidi kuvipa kipaumbele vikundi vyao vya ujasiri mali kwa kuvipatia mikopo isiyokuwa na riba Pamoja na kuwatafutia masoko ili wajikwamuwe kiuchumi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: