Saturday, 12 September 2020

UDART WAJIVUNIA MAFANIKIO UONGOZI WA MAGUFULI


NA HERI SHAABAN
KAMPUNI ya Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam UDART wajivujia mafanikio utekelezajj wa majukumu yake katika uongozi wa Rais  Magufuli.

Akizungumzia mafanikio ya Kampuni hiyo Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART  Sabato Kosuri alisema kampuni hiyo ni ya kwanza Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma za uendeshaji wa mabasi yaendayo haraka.


Kosuri alisema  mradi huo  umesaidia kutunza mazingira hapa ya Dar es Salaam kwa kuwa uwepo wa mabasi yaendayo haraka kumepunguza idadi ya mabasi madogo (Daladala)katika mkoa huo.

"Tunajivunia mafanikio katika uongozi wa  Rais wetu John Magufuli kampuni yetu imefanya mambo makubwa katika kutoa huduma ya usafiri" alisema Kosuri.


Kosuri alisema kwa sasa serikali inaendelea na maboresho katika mradi huo ili kufikia malengo yake na matarajio ya wananchi wa mkoa wa Dar es salaam.

Aidha alisema kwa sasa UDART inahudumia wastani wa abiria 200,000  kwa siku sawa na   ongezeko la asilimia 295   kutoka abiria 56,000 ulipoanza mradi mwaka 2016.

Akizungumzia changamoto iliyokuwepo kwa sasa UDART uchache wa mabasi kulinganisha na muitikio na uhitaji wa sasa,mabasi yaliopo kwa sasa yanatoa huduma hayatoshelezi kulinga na idadi ya wasafiri inaongezeka kila siku kutokana na huduma bora na za haraka katika mradi huo ambapo kwa sasa upo chini ya uangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina .


Alisema Mkakati wa Serikali  kwa sasa kuboresha huduma za BRT ikiwa pamoja kuongeza idadi ya mabasi ili kuendana na uhitaji halisi kwa sasa.

" Katika mafanikio pia changamoto mbalimbali  zipo ikiwemo elimu ya matumizi ya miundombinu ya mradi hasa barabara,baadhi ya waendesha vyombo vya moto kuingia kwenye barabara za mwendokasi changamoto ambayo inapelekea ajali na ucheleweshaji wa huduma,ambapo katika mabadiliko yanayoendelea kwa sasa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya miundombinu hiyo


Akizungumzia mikakati mingine ya serikali kuboresha huduma ya mawasiliano ndani ya mabasi na mwenye vituo vya MwendoKasi.

Mwisho

No comments:

Post a comment