NA HERI SHAABAN
MGOMBEA udiwani wa chama cha Mapinduzi CCM Sharik Choughule amesema akichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Kivukoni katika uongozi wake miaka mitano ataleta maendeleo makubwa kuijenga kata hiyo  kuwa ya kisasa.

Sharik aliyasema hayo Kata ya Kivukoni  leo wakati wa akipita katika soko la samaki la Feri kuomba kura za Mh Rais John Magufuli na Mgombea ubunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa tiketi ya CCM.


"Mkinichagua kuwa Diwani wa Kata hii nitaboresha miundo mbinu ya Soko la Samaki la Feri soko liwe la kisasa na kuongeza   fursa   mbalimbali  kwa wafanyabiashara ikiwemo kuvipatia vikundi vyote mikopo ya Serikali inayotolewa ngazi ya Halmashauri ya Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu " alisema Sharik.


Sharik alisema   Kata ya Kivukoni imepata bahati kubwa sana ina kitega uchumi soko la kisasa     hivyo kila mwananchi wa kata hiyo siku ya Octoba 28/2020 apige kura ya udiwani kwa Sharik,ubunge Mussa Zungu na Rais wetu John Magufuli .

Alisema Rais John Magufuli amefanya mambo makubwa katika uongozi wake katika nchi yetu kuelekea Tanzania ya Viwanda ambapo kwa sasa tumefikia uchumi wa kati ameweza kuboresha miundo mbinu ya Reli ya kisasa,kununua ndege kujenga barabara  kuboresha sekta ya afya nchi nzima.

Aidha alisema mambo mengine yaliofanya na Rais kuboresha soko la samaki feri ,Mkakati ya elimu bila malipo yote yamefanywa na  John Magufuli sasa hivi watoto wetu wanasoma bila kulipa ada

 Sharik alisema atashirikiana na wafanyabiashara wa soko la Kimataifa la Feri pamoja na Wafanya biashara wa soko hilo katika mambo mbalimbali kila wakati hivyo wasiwe na wasiwasi   katika shughuli za uzalishaji na uvuvi   wote waendelee kukiamini chama chao cha Mapinduzi CCM kwa maendeleo endelevu.


Aliwakikishia kuwapatia mikopo ya serikali wafanyabiashara wote wa Mama Lishe na Baba Lishe wa wanaofanya shughuli katika soko hilo  wamchague kwa kishindo ili aweze kuwa diwani awasimamie mikopo hiyo  ajili ya vikundi vyao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: