Mwanasheria wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT)  Glorious Luoga akizungumza na viongozi wa mila katika kata ya Eslalei iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) Jeremia Wambura akisalimiana na mjumbe wa bodi ya Chama hicho Lekule Laizer baada ya kuwasili wilayani Monduli kwa ajili ya mkutano na wazee wa Mila (Malaigwanani).
Wazee wa Mila wa kabila la kimasai(Malaigwanani) ambao pia ni wafugaji wakimsikiliza mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania Jeremia Wambura.


CHAMA Cha wafugaji Tanzania(WCCT) kimetoa rai kwa  maofisa mifugo wa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia Nyanda za malisho kwenye wilaya zenye mfugaji ili kuepusha migogoro kati ya wafugaji na wakulima.


Aidha kimewataka ofisa  mifugo hao kuhakikisha wafugaji wanaopeleka mifugo yao kwenye minada kutotozwa ushuru wa mifugo ikiwa wafugaji hawajauza mifugo yao.

Kauli hiyo imetolewa na mwanasheria wa chama hicho Glorious Luoga wakati akizungumza na viongozi wa mila pamoja na wafugaji katika wilaya ya Monduli iliyopo mkoani Arusha.

"Nimesikia malalamiko ya wafugaji kwamba halmashauri imepanga mpango wa matumizi bora ya ardhi lakini bado maeneo ya nyanda za malisho yanavamiwa hali inayosababisha mifugo kukosa malisho. Niwaombe maofisa mifugo kuanzia ngazi ya halmashauri mpka  ngazi ya kata kuhakikisha mnashirikiana na wafugaji kuhifadhi nyanda za malisho".


Kuhusu mifugo kutozwa ushuru ambayo haijauzwa mnadani alisema ni kosa kisheria na kuwataka maofisa mifugo hao kutatua kero hiyo mara moja kwa kuwa ni kilimo cha wafugaji wengi kulazimishwa Kutoza mifugo iliyokosa soko wakati wa kuirudisha nyumbani.

Wakili Luoga alitumia fursa hiyo kuwaasa wafugaji kuwa na Mahusiano mazuri na watumishi wa umma kwa ajili ya ustawi wa mifugo yao.


Naye mwenyekiti wa CCWT Taifa Jeremia Wambura alisema  atasimamia na kutetea haki zote za wafugaji kwa kuwa ni sekta muhimu hapa nchini inayochangia pato la Taifa.

Amesema katika kipindi chake cha uongozi ataanzisha viwanda vya kusindika mafuta ikiwa ni pamoja na kuchimba visima kwenye maeneo yote ya nyanda za malisho hapa nchini yaliyorasimishwa ili wafugaji waondakane na adha ya kukosa malisho na migogoro ya kugombania malisho.


"Katika kipindi changu cha uongozi nitahakikisha wafugaji wanafuga kwa tija kwa kuanzisha viwanda vya kusindika maziwa pamoja na kuchimba visima kwa ajili ya kumwangalia Nyanda za malisho kwa maeneo yote yaliyopimwa na serikali ili mifugo malisho ya uhakika".



Awali wakizungumza kwenye kikao hicho Julius Loibos, Yamat Laizer na Oleiboku Ole Kisambu walidai kuwa nyanda za malisho Zina akiwa licha ya uwepo wa mpango wa matumizi bora ya ardhi na Hakuna hatua zozote zinachokuliwa dhidi ya wavamizi hao.

"Tuna changamoto nyingi katika sekta ya mifugo ikiwemo chanjo za mifugo, maeneo ya malisho kuvamiwa pamoja na kulazimishwa kulipa ushuru wa mifugo tunayoipeleka mnadani hata kama hatujauza pindi tunapotaka kuirudisha majumbani".

Akijibu hoja hizo ofisa mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Ommary Sanga aliahidi kushughulikia kero ya maeneo ya Nyanda za malisho kuvamiwa kwa kushirikiana na Idara ya ardhi.

Kuhusu ushuru alikiri wafugaji ambao bawajahza mifugo kutonzwa ushuru kwa kuwa hawaombi vibali kwa maofisa mifugo wa kata vya kupeleka mifugo yao na kwamba kuanzia sasa mifugo iliyopelekwa mnadani na kukosa soko haitatizwa ushuru.

"Ni kweli Kuna upungufu wa malambo ya mifugo kunywea maji kutokana na Bajeti ndogo inayotengwa na halmashauri kwa kuwa fedha zinazopatikana zinatumika kujenga mabwawa ya kipaumbele".

Share To:

msumbanews

Post A Comment: