Tuesday, 22 September 2020

Mtega awaomba wananchi wamtume kutatua kero zinazowakabili


MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbarali kupitia chama cha mapinduzi,Francis Mtega ameomba wananchi  wa wilaya hiyo wamtume akawawakilishe na kuwa  amelelewa na chama cha mapinduzi na kukomaa na kujifunza mengi  ndo sababu ya chama kimemwamini na kumteua.

Amesema hayo juzi kwenye mkutano wa kampeni katika kitongoji cha Mtakuja katika kata ya Ubaruku.

Mtega amesema kuwa katika   mchakato wa kumpata.mgombea mmoja ulikuwa mkubwa ambapo  walikuwa watia 37 ambao wote kwa pamoja wanamuunga mkono katika kampeni na wengine wamerudi makazini lakini wapo pamoja nae.

Aidha Mtega amesema anapokea ushauri kila siku namna ya kuendeleza wilaya ya mbarali hivyo hana shaka kutokana na kuwa na jeshi kubwa nyuma yake.

No comments:

Post a comment