Tuesday, 1 September 2020

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA KAMPENI WILAYA YA ILALANA HERI SHAABAN
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu kuzindua Kampeni za Ubunge Wilayani Ilala Septemba 5.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za CCM Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala  Said Sidde alisema,uzinduzi wa Kampeni za  ubunge Wilaya ya Ilala,zitazinduliwa  Jimbo la Segerea   siku ya Jumamosi viwanja vya Tabata Shule kuanzia saa mbili asubuhi ambapo mgeni rasmi Mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu.

"Kampeni zetu za ubunge na udiwani CCM wilaya ya Ilala tunazindua Jumamosi Septemba 5  mgeni rasmi   mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu nawaomba wana CCM wote tujitokeze kwa wingi viwanja vya TABATA shule shughuli yetu itaanza asubuhi saa mbili "alisema Sidde.

Aidha Sidde alesema kampeni hizo kwa Jimbo la Ukonga zitazinduliwa Septemba 6 Viwanja vya Kampala kuanzia saa mbili asubuhi .


Alisema Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Ilala  kinapeperusha bendera yake ya CCM kwa kuwanadi wagombea udiwani wa kata zote 36 na wabunge wa jimbo la Segerea Bonah Ladslaus,Ukonga Jerry Silaa na jimbo la Ilala Mussa Zungu.

Alisema chama hicho kimejipanga vizuri kitashinda majimbo yake yote ya uchaguzi wilaya ya Ilala

Mwisho

No comments:

Post a Comment