NA HERI SHAABAN
MGOMBEA wa udiwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto   amendelea kumwaga sera za CCM katika kuomba kura huku akijizolea wanachama wa CUF kujiunga chama cha Mapinduzi CCM kutoka Kata ya Vingunguti Manispaa ya Ilala

Akipokea wanachama wapya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma,alisema hayo ni mafanikio mazuri ndani ya chama Mapinduzi    CCM kuendea kuzoa wanachama wa upinzani sera za CCM zinakubalika , wagombea wanakubalika  na CCM itashinda kwa kishindo.


Akizungumza  mambo aliyofanya   katika Kata ya Vingunguti  Omary Kumbilamoto alisema katika uongozi wake wa miaka mitano iliyopita ameboresha huduma za afya ndani ya kata hiyo kwa kununua vifaa vya kisasa  zahanati ya Vingunguti pamoja na kuwakabidhi gari la wagonjwa ambayo inatumika mpaka sasa ,sekta ya elimu wanafunzi wanakula mlo wa mchana pamoja na kuwawekea maji safi na salama kwa ajili ya kunywa shule zote .


Omary Kumbilamoto alisema mambo mengine ambayo amefanya  katika kata hiyo   kuboresha Ofisi za CCM  za kata na matawi  kwa sasa zinavutia .

Aliwataka wananchi wa Kata hiyo wamchague Rais John Magufuli wampigie kura kwa kishindo pamoja na Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli ili waweze kuwaletea maendeleo .

" Nawaomba wananchi wenzangu wa Vingunguti kura yangu ya Udiwani ,kura ya Rais John Magufuli    na Mbunge wangu Bonah Ladslaus Kamoli ili tuweze kuibadilisha Kata hii iwe ya kisasa   zaidi
Serikali ya awamu ya tano imewaletea Machinjio ya Kisasa ni juhudi za Rais wetu John Magufuli na Bonah Kamoli katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda  "alisema Kumbilamoto

Alisema mikakati yake mingine ndani ya kata  Vingunguti akichaguliwa atawajengea barabara za kisasa katika mradi wa Serikali DMDP kwa ajili ya kuboresha miundombinu ,kutoa ajira 300 kwa wakazi wa Vingunguti na kata za jirani mara baada machinjio hayo ya kisasa kukamilika  .

Pia alisema mikakati mingine kuwajengea soko la nyama taratibu zimeshafanyika nyumba 20 zitabomolewa kwa ajili ya mpango huo kuanza dhumuni kuongeza ajira kwa wananchi wa Vingunguti  Manispaa ya Ilala.


"Siku ya Octoba 28 ni siku ya Mapumziko tujitokezeni tukapige kura wananchi wote wa Kata hii ya Vingunguti  na mkinichagua kwa awamu ya pili kuwa diwani wa kata hii nitatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM na mkakati wangu mwingine nitawakabidhi gari kwa ajili ya kubebea maiti na kusafirisha misiba .

Akielezea wimbi la kupokea wanachama kutoka vyama vya upinzani alisema jana wamepokea wanachama 20 kutoka chama cha wananchi CUF Kariakoo Mtaa wa Mtambani na Juzi wamepokea wanachama 70 kutoka Mtaa wa  Majengo tawi Geto boys na kufanya jumla ya wanachama 90 ndani ya mwezi mmoja ambao wamerudi CCM kuunga mkono juhudi za chama hicho.

Kwa upande wake Kada wa CCM Philipo Mpemba aliwataka wagombea wa vyama vya upinzani katika Jimbo la Segerea  wanapokuwa Jukwaani watoe sera za vyama vyao wasingilie maisha ya watu sio vizuri.

Mpemba alisema wagombea wa CCM wanapokuwa jukwaani wanatoa sera za chama hicho na kuelezea utekelezaji wa Ilani aijawai kuwachafua wapinzani.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: