NA LILIAN JOEL, KITETO

CHAMA cha wafugaji Tanzania (CCWT) kimesema kitawasilisha hati ya dharura mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ya kuitaka Kampuni ya Mkungunero Game Reserve  iliyopo wilayani Kondoa mkoani   humo kuheshimu tamko la Rais  John Magufuli la kutaka wananchi wanaoishi pembenzoni mwa hifadhi kutobughudhiwa.

Aidha chama hicho kimeitaka kampuni hiyo ya Mkungunero kumlipa mara moja ng'ombe 214  wa mfugaji Lenina Satulu

Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa CCWT Taifa Jeremia Wambura wakati akizungumza  na wafugaji wa Kijiji cha  Irkiushiobor  kilichopo wilayani Kiteto ambao  walimlalamikia kuwa kampuni hiyo ya Mkungunero inawapiga na kuwatesa wananchi pamoja kuwapora mifugo yao bila sababu za msingi.

"Kwa sababu waraka wa tamko la  Rais Magufuli upo Mkungunero hataki kuheshimu waraka huo, tutawasilisha hati ya dharura mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ya kutaitaka Mkungunero kbsmu tamko la Rais mpka  hapo litakapotamkwa vingine yao".

Amesema haiwezekani Rais Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa nchi atoe tamko halafu uongozi wa Mkungunero ukaidi tamko hilo na kwamba njia rahisi ya kuwasaidia ni kuwaburuza mahakamani.


Kuhusu ng'ombe wa Satulu  alisema uongozi wa Mkungunero aidha kwa hiari au kwa lazima ng'ombe wa   Satulu lazima walipwe kama huku u ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ilivyoelekeza.

"Wapelekeeni salam Mkungunero kwamba wasiyependa kaja wa take wasitake watalipa ng'ombe wote wa Satulu haiwezekani mahakama ielekeza kwamba mfugaji huyu alipwe ng'ombe 214 halafu wao wamlipe ng'ombe 96 pekee huu ni uonevu ambao sisi kama CCWT hatutakubali".


Awali akizungumza kwa uchungu Lazaro, Le Baraka kutoka Kijiji cha Kati alidai kuwa askari wa pori la Mkungunero wamekuwa walikamata mifugo ya wananchi kwenye maeneo ya vijiji kisha kuiswaga na kupeleka ndani ya hifadhi yao ili mifug hiyo ilipiwe fidia na wakati mwingine wanaitaifisha.


Kotete Ndaramani kutoka Kijiji cha Irkiushiobor alisema uongozi wa Mkungunero umekuwa ukiwatesa wananchi na kwamba hivi karibuni walikamatwa wananchi wakiwa kanisani na kudai kuwa wameingia ndani ya hifadhi lakini pia walimkamata mama mjamzito akipita barabara I na kufunga nyumba ya gari na kumburuza hadi mimba ikatoka.

Alisema watoto  walikamatwa wakichunga mifugo wanawapigwa na baadhi yao kuuwawa huku wakilazimishwa kula maganda ya nyoka hali ambayo imesababisha watoto kupata madhara makubwa.


"Tunajiuliza Mkungunero ni nchi nyingine nje ya Tanzania kiasi cha kukaidi agizo la Rais???? Tunaomba mahali popote Rais Magufuli alipo asikie kilimo chetu dhidi ya uongozi wa Mkungunero kwa sababu sisi hatuna nchi nyingine ya kwenda hatuna maeneo ya malisho wala Makazi kutokana na Mkungunero kumega eneo la Kijiji kila wakati".


Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kiteto, Ofisa Tarafa wa Tarafa  ya Makame Ibrahim Ole Mario alikiri  uwepo wa Mgogoro baina ya wananchi hao na pori la Mkungunero na changamoto kubwa wananchi hao walikamatwa wanaopeleka wilayani Kondoa mkoani Dodoma.



Ofisa ardhi na mali asili kutoka wilaya ya Ngorongoro Dorcus Gama alisema kwenye ramani ya wilaya ya Kiteto hakuna sehemu inayoonyesha kwamba Mkungunero ipo ndani ya wilaya ya Kiteto.


"Kwenye ramani yetu ya wilaya hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Mkungunero ipo ndani ya wilaya yetu na tunachojua sisi ni kwamba Mkungunero ipo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma na tume iliyoundwa na Rais ilikuja hapa kushughulikia Mgogoro huu wa mpaka lakini majibu bado hayajatolewa".

Akizungumzia malalamiko hayo  meneja wa Mkungunero Khadija Malongo alisema yupo kikaoni na kwamba Hawezi kutoa ufafanuzi wowote kuhusu malalamiko ya wananchi hao.



Ooooooooooooooooooooooooooooooo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: