Tuesday, 1 September 2020

ARUSHA FESTIVAL YAWEKA REKODI ,WASANII WAMPONGEZA DC KIHONGOSI

Na Woinde Shizza, Arusha

Wananchi wa jiji la  Arusha pamoja na wasanii  wamepongeza mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi pamoja na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli   kwa kuwajali Vijana  na kuwakutanisha pamoja katika tamasha la Arusha Festival ambapo walisema kuwa  hawana Cha kuilipa Serikali Bali watawashukuru kwakuwapigia Kura za kishindo katika uchaguzi huu.

Walimshukuru Rais kwakuwaletea kiongozi ambaye anajali vijana ,wamama na wazee kwani mbali na Tamasha hili pia mkuu  wawilaya aliweza kutoa magunzo ya ujasiriamali kwa wananchi bure kwa wananchi wote wa mkoa wa  Arusha na Sasa ameweza kuwakutanisha wasanii wote wa mkoa huu na kuwaambia kuwa mziki Ni ajira jambo ambalo limeweka history kwani hakuna kiongozi yeyote alieweza kufanya kitu Kama icho.

Akiongea na Mwandishi wa habari hizi  mmoja wawasanii wakongwe kutoka mkoani Arusha Jakobo Makala (JCB) alisema kuwa yeye Ni mkogwe katika tasnia hii ya mziki lakini hakuna kiongozi yoyote ambaye alishawahi kuwakutanisha wasanii wa Arusha na kusikiliza changamoto zao pamoja na kuzitatua Kama vile anavyofanya  mkuu huyu wa wilaya ambapo alimpongeza na kumtaka asihishie hapa Bali aendelee kuwapa mafunzo pamoja na kuwakutanisha

"Kwanza niseme watu wengi walikuwa wanazani usanii Ni uhuni lakini sio Hivyo Bali usanii ni ajira kwa zilivyo zingine na iwapo ukiufanyia usanii wako kwa kuutilia manani lazima utakutoa na kukupafaida,nachoweza kusema kwa wasanii wa mkoa wa Arusha wamepata bahati waitumie vyema bahati hii wasiichezee"alisema  msanii kutoka Dar anaejulikana kwa jina la Beka

Alisema kuwa Arusha Kuna wasanii  na kunavipaji ,Ila aliwataka wafate Sheria wawe na heshima kwa kilamtu pia wafanye kazi kwa juhudi huku akiongeza  kuwa Ni vyema pia wakawa  wavumilivu na kuwaambia kuwa hakuna msanii anaeweza kutoka bila  kuvumilia pamoja kujituma Sana na  hauwezi kuwa msanii Kama hujitumi pia huwezi kujiita msanii Kama unanyimbo moja hivyo aliwasisitiza wajitume zaidi kwani hata wao wasanii wa Dar wananituma


Akiongea wakati wa kufungua na kufunga tamasha Hilo lililoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya , Mkuu wa wilaya ya Arusha  Kenani Kihongosi aliwaahidi Kuwapa ushirikiano zaidi  huku aliwataka wasanii hao na wananchi kuzidi kuiunga mkono serikali kwani serikali inaamini Sanaa Ni Ajira.

Alisema tamasha hili Ni matokeo ya Kikao alichofanya na wasanii hao mapema mwezi agost mwaka huu na ndipo alipoamua kuwakutanisha pamoja na kusikiliza kero ambapo aliwataka wasanii hao kutumia vipaji vyao kwa kujipatia vipato na kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla.


"Tamasha hili limewakusanisha  wasanii wa mkoa huu zaidi ya 70 pia tumeweza kiwaalika baadhi ya wasanii kutoka jiji la dar es salaam akiwemo Marioo,Beka,Dogo janja na wengine hii Ni njia moja wapo yakuwaleta pamoja wasanii Hawa na hatutaishia hapa tutaendelea kuwakusanya wananchi na wasanii ilikuwaeleza fursa mbalimbali zilizopo apa nchini kupitia tasnia zao naniseme mbali na hapa pia nimeanza kuandaa tamasha la Wafanya mazoezi kutoka klabu zote za jiji la Arusha pamoja na vikundi vyote nitakapo kamilisha nitawatangazia "Kiongosi

Alisema mikakati iliyopo katika Mkoa katika kukuza tasnia ya michezo ni kuhakikisha Mkoa unapata timu ya ligi,pia tayari kuna programu ya kukimbia kila Jumamosi,Mkoa umepata bendi ya muziki wa dansi na sasa kuna huo mpango wa kuibua na kukuza vipaji vya wasanii wa bongo fleva
No comments:

Post a Comment