Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kushoto na team ya wataalam na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Jeshi la magereza mkoani hapo, akikagua vifaa katika kiwanda cha ngozi cha Karanga mkoani hapo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akibeba tofali na kupeleka katika
jengo jipya linaloendelea kujengwa katika kwanda cha ngozi cha
karanga Mkoani kilimanjaro.
Wafugaji
katika kijiji cha Miti Mirefu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro
wametakiwa kulipa deni la kiasi cha Shilingi Milioni kumi na tisa,
wanalodaiwa na Serikali ikiwa ni faini iliyotokana na kukiuka mkataba wa
kuingiza mifugo kwa ajili ya malisho katika ranchi ya West Kilimanjaro,
inayomilikiwa na Shirika la Ranchi zaTaifa (NARCO).
Hatua
hiyo imechukuliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina
alipofanya ziara katika Ranchi hiyo na kusikiliza changamoto
zinazowakabili wafugaji katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo
dogo la kulishia mifugo,josho nazahanati kwa ajili ya matibabu yao.
Baada
ya kuwasilisha changamoto ya eneo la kulishia mifugo ndipo Waziri Mpina
alipoongea kwamsisitizo kuwa“ Mmekiuka mkataba mlioingia na Serikali
baada ya kupewa kibali cha kulishia mifugo katika ranchi ya Taifa,deni
la shilingimilioni 19 lilipwe ndani ya siku kumi na tano (15) na
lisipolipwa mkataba uvunjwe, hizini maliza Serikali hatuwezi kuziendesha
kwa namna ambavyo kila mtu anataka.” Alisema.
Akitoleaufafanuziswalala
josho, Waziri Mpina alisema hakuna maelezo ya kutosha kwa nini josho
la zamani halijakarabatiwa na kuagiza Taasisi ya Tafiti za Mifugo
(Tariri) kukarabati josho hilo kwa siku kumi na tano na kusema kuwa
baada ya zoezi hilo serikali itawaletea wafugaji dawa za ruzuku za
kuogeshea mifugoyao.
Kwa upande wa Changamoto ya zahanati,
Mpina ameelekeza Shirika la Ranchi zaTaifa (NARCO) kukarabati jengo moja
chakavu ili liweze kutumika kama zahanati katika kijiji hicho na Mkuu
wa Wilaya hiyo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri kuleta wataalam na
madawa tiba.
Waziri Mpina alisema ili kuweza kuwasiadia
wafugaji hao kupata suluhisho la kudumu la eneo la malisho upatikane
muda wa kutosha wa kulifanyia kazi swala hilo ili liweze kupatikana
eneo la uhakika na la kudumu .
“Ni kazi ya Serikali kuhakikisha
Changamoto hizo za wafugaji zinatatuliwa kwa wakati kama
tulivyofanikisha kupunguza gharama za chanjo za mifugo kutoka shilingi
elfu moja (1,000/-) mpakaelfutano (5,000/-) hapoawali mpaka shilingi
miatano (500) kwasasa, sambamba nakushusha gharama za kuogesha mifugo
ambazo kwa sasa kuosha ngombe mmoja ni shilingi hamsini (50) na mbuzi
na kondoo ni shilingi ishirini (20), kwa hivyo hiyo changamoto ya
mipaka itashughuliwa na wataalam kutoka wizara husika.” Alisema.
Awali,
Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kuchataka ngozi kinachomilikiwa
na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya hifadhi ya jamii ya
(PSSSF )kilichopo Karanga mjini Moshi na kujionea vifaa vya
uzalishaji vilivyopo katika kiwanda hicho na namna ujenzi unaendelea na
kuwataka kumaliza shughuli hizo za ujenzi kwa wakati ili kuanza
uchakataji na uzalishaji utakaoliletea Taifa tija kwa kuuza bidhaa
zitokanazo na ngozi nje ya nchi na kongeza pato la Taifa.
“Tunawauzia
ngozi za ng’ombe wetu wanakuja na bidhaa kamaviatu,mapochi na mikanda
na kutuuzia bei ghali wakati sisi wenyewe tuna uwezo wakuzalisha
bidhaa hizo hapa nyumbani na kuwauzia wao,wakati umefika sasa wa sisi
kutumia zao hili la mifugo kuliongezea pato Taifa.” Alisema.
Kwaupande
wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara kutoka Bank yakilimo (TADB)
Bw. Jeremiah Mhada amesema kwa sasa bank hiyo inafanya kazi kwa karibu
na shirika la Ranchi zaTaifa NARCO hii ni katika kuhakikisha kwamba
ranchi hizo zinaweza kujiendesha kibiashara na tayari wameshapokea
maombi ya mkopo kutoka ranchi ya Kongwa Dodoma na wanayafanyia kazi.
Ziara
hiyo ya Waziri Mpina Mkoani Kilimanjaro ni matokeo ya utekelezaji wa
majukumu yake katika kuendelea kuimarisha na kuboresha sekta ya mifugo
na uvuvi nchini.
Post A Comment: