Mkurugenzi wa Selcom Tanzania Sameer Hirji akimjazia mafuta moja ya washindi wa kampeni ya Achana na Cash, lipa kidijitali tukupige Full tenki iliyokuwa inaendeshwa na Kampuni ya Selcom pamoja na Puma Energy, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhalla
 Mmoja ya washindi wa Kampeni ya Achana na Cash, lipa kidijitali tukupige Full tenki, Paulo John akiwashukuru kampuni ya Selcom kwa kuanzisha kampeni hiyo na kuwaasa watanzania kutumia mfumo wa kidijitali kwenye malipo kwani una faida kubwa sana na inaepusha msongamo.
 Moja ya washindi akihakikisha gari yake inajaa mafuta
 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhalla akimjazia mafuta moja ya washindi wa kampeni ya Achana na Cash, lipa kidijitali tukupige Full tenki iliyokuwa inaendeshwa na Kampuni ya Selcom pamoja na Puma Energy, Kulia ni Mkurugenzi wa Selcom Tanzania Sameer Hirji.


KAMPUNI zalendo za Selcom na Puma Energy, leo tarehe 13 Agosti zimeendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania kurasimisha malipo hasa katika sekta ya nishati. Kampuni hizo zimefanya hivyo kwa kuendeleza kampeni yao ya “Achana na cash, lipa kidijitali tukupige full tenki” kwa muda wa wiki mbili za ziada mpaka 31 Agosti 2020. 

Kampeni hiyo ilianza tarehe 4 Juni na kupangwa kuisha tarehe 4 Agosti 2020. Aidha kutokana na muamko mkubwa wa wateja, kampuni hizo zimeamua kuendeleza kampeni hiyo ili kuwapa Watanzania wengine 10 fursa ya kuzawadiwa full kwa kulipa kidijitali katika vituo vya Puma Energy.

Hayo yamebainika katika halfa fupi ya kuwazawadia full tenki washindi 10 wa awamu ya kwanza iliyofanyika katika kituo cha Puma Energy Upanga. Akigongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Selcom, Baguma Mpenda amesema kwamba dhamira kuu ya kampeni hiyo ni kuhimiza Watanzania kuendelea kufanya malipo kidijitali kupitia SelcomPay Mastercard QR kwani ni rahisi na salama zaidi na si kuwashindanisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania,  Dominic Dhalla alisema “Puma ni kinara wa malipo ya kidijitali nchini ukilinganisha na makampuni mengine ya nishati ya mafuta. Tuna njia zaidi ya moja za malipo ya kidijitali zikiwema SelcomPay Mastercard QR na Puma Elite Card ambazo zinatumika katika vituo vyetu vyote nchini.”

Dhamira ya kampuni hizi kurasimisha malipo ni dhahiri kwani siyo mara yao ya kwanza kuendesha kampeni kama hii kuhimiza malipo ya kidijtali. Mnamo Novemba 2019 ziliendesha kampeni ya Bomba Weekends ambayo iliwapa wateja waliolipa kidijitali kupitia SelcomPay Mastercard QR rejesho la 5%.

“Tumeona ongezeko kubwa la malipo ya kidijitali ndani ya miaka michache iliyopita. Kikubwa na muhimu ni kwamba Watanzania wanaendelea kuibeba dhamira ya serikali ya kurasimisha uchumi wa nchi yetu kwa kufanya malipo kidijitali. Tumeona hili si kwa Puma na sekta ya nishati tu, bali pia katika sekta zingine tunazojihusisha nazo. Kazi yetu kama Selcom ni kuboresha na kurahisisha teknolojia hii ya malipo hadi kumfikia kila Mtanzania. Tunataka kufika wakati hadi machinga waweze kupokea malipo na kufanya matumizi wakihitaji kupitia SelcomPay/Mastercard QR.” Alisema Mkurugenzi wa Selcom,  Sameer Hirji.

Akiongea katika hafla hiyo, mmoja wa wazawadiwa hao Washngton Onyango alisema anavutiwa kutumia huduma ya SelcomPay/Mastercard QR kwa sababu ni rahisi, salama na haina makato yoyote kwa mteja kama ada ya kukamilisha muamala. “Unalipa kama ilivyo na uzuri ni kwamba inapokea malipo kutoka mitandao yote ya simu na baadhi ya mabenki.” Aliongeza Onyango.
Share To:

Post A Comment: