Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole  Senare akiangalia vipando alipotembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  kujionea teknolojia mbalimbali zinazofanywa na watafiti wa Chuo hicho kwa faida ya Wakulima na wafugaji wa Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole  Senare akipata maelezo alipotembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA . 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole  Senare akipata maelezo alipotembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA . 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole  Senare akipata maelezo alipotembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA .
 Maelezo yakitolewa kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole  Senare alipotembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA .


Na Calvin Gwabara, Morogoro


MKUU wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole  Senare  leo ametembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA yeye mwenyewe Binafsi kujionea teknolojia mbalimbali zinazotakiwa na watafiti wa Chuo hicho kwa faida ya Wakulima na wafugaji wa Tanzania.

Mhe. Senare amefanya ziara hiyo binafsi ili kupata nafasi ya kujifunza kwa kina badala ya kutegemea zile ziara rasmi zinazoandaliwa na Wasimamishi na watatu I wa maonesho kwenye maonesho hayo ka Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro.


Katika ziara hiyo amevutiwa na kazi nzuri inayofanywa na watafiti wa SUA katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za Wakulima na wafugaji na kuongeza tija.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro amesema Mkoa wa Morogoro umepata bahati ya kipekee ya kuwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA hivyo Mkoa na Wakulima hawana budi kuwa tumia wataalamu wa chuo hicho katika kuboresha Kilimo na ufugaji wao.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kuamua kuongeza muda wa maonesho hayo kwa siku mbili hii utawapa wadau wengi nafasi ya kutembelea maonesho hayo na kujifunza lakini sisi kama Mkoa tunataka kuanzisha utaratibu ambao tutakuwa na maonesho yetu ukiacha haya ya nanenane ili watu wengi zaidi wajifunnze badala ya kusubiria nanenanen tuu” Alibainisha Mhe. Senare.

Hata hivyo pia baada ya kujionea mambo mazuri kwenye banda hilo la SUA ameahidi kuileta familia yake yote kutembelea maonesho hayo hasa banda la SUA ili waweze kujifunza na kuweza kulima na kufuga kisasa na kuongeza tija.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kinashiriki maonesho ya Kilimo nanenane kitaifa Mkoani Simiyu na pia Kikanda kwenye Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro.


Share To:

Post A Comment: