NA HERI SHAABAN.

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija ametoa maagizo kwa Mkandarasi wa Barabara ya Tabata Kimanga kufika ofisini kwake na mpango mkakati wa ujenzi wa barabara hiyo ambayo umetelekezwa kwa muda mrefu.

Mkuu wa Wilaya Ludigija aliyasema hayo katika ziara yake  endelevu ya kukagua miradi ya maendeleo halmashauri ya Ilala ikiwemo miradi ya DMDP  ya jimbo la Segerea na Jimbo la Ukonga .
"Dhumuni la ziara yangu kukagua miradi ya maendeleo iliyopo halmashauri ya Ilala   nimekuta ujenzi wa barabara hii ya Kimanga  ujenzi wake sijalidhishwa nao nakuagiza Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala andika barua ya wito Ijumaa aje na mpango mkakati wa ujenzi wa barabara hii ,pia aseme kwanini amekwamisha ujenzi kwa muda mrefu kupelekea kero kwa Wananchi " alisema DC  ILALA  Ludigija 

Amemwomba Mkandarasi huyo kufika Ofisi  ya Wilaya ya Ilala na ujenzi wake uwanze   mara moja kuondoa kero hiyo.

Wakati huohuo amepongeza ujenzi wa miradi ya DMDP   ikiwemo soko la Bombom ambapo alitoa agizo Soko la  kisasa Bombom likabidhiwe Manispaa ya Ilala  Mwisho wa mwezi huu wafanyabiashara waanze kazi ndani ya soko hilo .


"Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala naomba simamia wafanyabiasha walengwa wa Kiwalani Bombom Agosti 30 Mwaka huu waanze biashara katika soko lao   kila mmoja akikisha anapata kizimba chake " alisema .

Katika hatua nyingine   amepongeza ujenzi wa daraja la Ulongoni A unavyoendelea ambapo unajengwa na mradi wa   DMDP amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi usiku na mchana kabla mvua za mwezi Octobar kuanza .

Alisema ujenzi wa daraja hilo ukikamilika utaondoa kero kwa Wakazi wa Gongolamboto na Ulongoni ,amepiga marufuku wananchi kuchimba mchanga katika bonde la Mto Msimbazi,amezitaka Kamati za Mazingira  kuanzia ngazi ya kata na Manispaa kuachukulia hatua wananchi wenye tabia ya kuchimba mchanga katika bonde la Msimbazi halmashauri ya Ilala.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: