BODI ya Nafaka na Mazao mchanganyiko,(CPB) tawi la Arusha imefungua kituo cha mauzo wilayani Same mkoani kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa sehemu ya mikakati ya bodi hiyo ya kufikisha bidhaa zao karibu zaidi na wateja.


Aidha wametoa msaada wa unga wa  mahindi, mchele na mahindi ya makande ya chapa Nguvu yanayozalishwa na bodi hiyo kwa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Mama Kevina kilichopo wilayani Same.



Akiongea wakati wa uzinduzi huo uliofanyika juzi, Kaimu meneja wa CPB, tawi la Arusha, Idd Mkolamasa kuwa wamejipanga kufungua vituo vya mauzo maeneo mbalimbali ya nchi ambapo tayari wameshafungua kituo kama hicho Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.


Alisema kuwa wana mwaka mmoja tokea wakabidhiwe kuendesha kinu cha kuchakata nafaka cha NMC, Arusha ambapo kwa kipindi hicho wameweza kutengeneza faida ya faida ya zaidi ya shilingi milioni 800 hivyo kuweka mipango ya kufungua vituo vya mauzo maeneo mbalimbali ili kusogeza bidhaa zao karibu zaidi na wateja.


Mkolamasa alitaja maeneo mengine wanayotarajia kufungua vituo  vingine vya  mauzo ni Horohoro mkoani Tanga, Tarakea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na Babati mkoani Manyara.



"Kwa kipindi cga mwaka mmoja tokea tukabidhiwe kinu cha kutakata nafaka cha Arusha kwenye biashara ya unga wa chapa Nguvu ambao dona bora na sembe bora  tumepata faida ya zaidi ya shilingi milioni 500 na kwenye maghala yetu tunayokodishia taasisi nyingine kuhifadhi nafaka zao tumepata faida ya zaidi ya milioni 300," alisema Mkolamasa.


Anasema sababu ya unga wao kupendwa ni namna wanavyouandaa kwa usafi na utaalam wa hali ya juu kwa kuhakikisha viini lishe vya protini na mafuta ambavyo ni muhimu katika kuujenga na kuupa joto mwili vinabaki.


"Unga wetu tunauzalisha kwa usafi wa hali ya juu ili kumlinda mlaji. Mara baada ya kuingiza mahindi kiwandani tunahakikisha tunayapitisha kwenye mitambo yetu kwa ajili ya kuyapembua ili kuondoa takataka zote ikiwemo mawe na misumari," alisema Kaimu Meneja huyo wa tawi la Arusha na kuongeza.


" Tukishahakikisha mahindi yako safi tunapitisha kwenye mashine maalum kwa ajili kurahisisha umenyaji wa ganda la juu wakati wa kusaga kisha tunayasafisha ili kuhakikisha yanakuwa safi kabisa,".



Mkolamasa alisema kuwa unga chapa nguvu unapatika kwenye ujazo tofauti wa kilo moja, tano, 10, 25 na 50 ambapo umekuwa ukiuzwa maeneo mbalimbali hapa nchini na nchi ya jirani ya Kenya ambayo ni moja ya wateja wao wakubwa kwani wamekuwa wakiuza unga wa mahindi pamoja na pumba.


MSAADA KITUO CHA MAMA KEVINA 


Kaimu meneja huyo wa CPB tawi la Arusha alikabidhi msaada kwa kituo cha mama Kevina ikiwa ni utekelezaji mpango wa taasisi hiyo kuisadia jamii.


Alikabidhi kituo hicho cha Mama Kevina  magunia 7  ya unga wa mahindi, magunia mawili ya mchele na mahindi ya makande kilo 50 ambapo bidhaa zote za zinazalishwa na CPB.


Mkuu wa kituo hicho, mtawa, Elizabeth Swai, alishukuru kwa msaada huo akieleza kuwa umewapa faraja wao na hasa watoto wanaowalea kwani unawaonyesha bado kuna watu wanawapenda na kuwajali.


Alisema kuwa kituoni hapo kuna watoto 31, lakini wanahudumia zaidi ya watoto 600 wenye ulemavu wa aina mbalimbali kutoka maeneo tofauti hapa nchini.


"Hapa mmewaona watoto wachache, ila sisi tunahudumia watoto wenye ulemavu wengi sana. Huwa wanakuja hapa kituoni na wazazi wao na wanakaa kwa siku 14 wakipatiwa matibabu na wataalam wa afya ambapo kwa kipindi hicho wazazi hulipia shulingi elfu tatu tu kwa ajili ya fomu ya matibabu," alisema mtawa, Eliza


Alisema gharama nyingine za matibabu ya watoto wenye ulemavu,  malazi na chakula kwa wazazi na watoto hulipiwa na kituo hicho jambo alilosema kuwa ni Mungu pekee anayewezesha mambo hayo kufanyika kwani wao hawana shughuli yoyote ya kuwaingizia kipato zaidi ya kilimo.
Share To:

Post A Comment: