Na John Walter-Manyara
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa wilaya ya Kiteto
mkoa wa Manyara ,imefanikiwa
kurejesha mahindi gunia 45 katika kijiji
cha Loltepes.
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya
Kiteto Venance Sangawe amesema mahindi hayo ni sehemu ya gunia 90 ambazo
Takukuru iliingilia kati kurejesha.
Sangawe amesema diwani wa kata ya Sunya aliemaliza muda wake, Musa Brayton na
mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi katika
kata hiyo Abdi Puputo walishindwa kutimiza masharti waliyokubaliana
na kijiji ya kulipa mahindi hayo baada ya kulima shamba la
kijiji ekari tisini.
Ameongeza kuwa makubaliano
kati ya watu hao na kijiji ilikuwa ni kulipa gunia moja kwa kila ekari tangu mwaka 2017 hivyo kwa kushindwa kufanya hivyo Takukuru
imeamua kuisaidia kijiji kurejesha mahindi hayo.
Akikabidhi mahindi hayo kwa
mwenyekiti wa kijiji cha Loltepes Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa, amewataka viongozi wa kijiji na shule kuhakikisha
mahindi hayo yanatumika kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za Loltepes
na Loiborsoit zilizopo katika kijiji hicho.
Huo ni mwendelezo wa
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara katika kurejesha na
kukabidhi mali kwa wahusika halali ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.
Post A Comment: