Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiangalia baadhi ya makatapila ambayo yameng’olewa betri zake na kuibiwa mafunta zaidi ya lita 100 na walinzi wa Kampuni ya ulinzi ya Hamseki Ltd inayolinda vifaa vya kammpuni ya Chico inayojenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbamba bay wilayani Nyasa ambapo ametoa agizo kwa jeshi la polisi mkoani Ruvuma kuwasaka watu walihusika na wizi huo.

Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami wa kampuni ya Chico inayojenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbababay wiayani Nyasa Waang Jun Yi kushoto,akimueleza jana Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Chiristina Mndeme kuhu iana na wizi wa betri na mafuta ya kuendeshea mitambo uliofanywa na walinzi wa kampuni ya Hamseki Ltd iliyopewa jukumu la kulinda vifaa vya mradi huo katika maeneo mbalimbali na hivyo kusababisha kazi za mradi kusimama.


Na Mwandishi Maalum,
Mbinga

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme,ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuwasaka na kuwafikisha mahakamani wafanyakazi wa kampuni ya Ulinzi ya Hamseki Ltd ya Songea,wanatuhumiwa kuiba vifaa vya kampuni ya Chico inayojenga barabara ya Mbinga hadi Mbambabay kwa kiwango cha Lami.

Wafanyakazi hao ambao ni walinzi wanahusishwa kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa Chico na kuiba mafuta zaidi ya lita 100 aina ya Disel na Betri 10 kwenye magari ya kampuni ya Chico katika kijiji cha Chunya wilayani Mbinga na hivyo kusababisha ujenzi wa mradi wa barabara kusimama .

Mndeme ametoa agizi hilo jana mara baada ya kufika katika eneo hilo na kushuhudia uharifu mkubwa uliofanywa na walinzi wa kampuni Hamseki Ltd ambapo ametoa masaa ishirini nne kwa jeshi la polisi kuwakamata walinzi hao ambao wamekuwa wakijihusisha na matukio ya wizi mara kwa mara.

Alisema, Rais Dkt John Magufuri ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ambao ni wenye manufaa makubwa kwa wakazi wa mkoa huo lakini baadhi ya watu wachache wanahujumu jitihada zinazofanywa na Serikali, kwa hiyo Serikali ya mkoa wa Ruvuma itahakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani.

Alisema, inasikitisha kuona Watanzania wenzetu ndiyo wanaohusika kuhujumu mradi huo ambao ukikamilika utachochea maendeleo na kurahisisha maisha ya wananchi wa wilaya ya Mbinga,Nyasa na mkoa wa Ruvuma.

Mndeme amehaidi kuwasaka wale wote walihusika na kuwachukulia hatua ili kukomesha vitendo vya wizi vinavyofanywa na baadhi ya watu wachache wasio utakia mema mkoa huo.

Amewataka watanzania wanaofanya kazi katika mradi huo, kufanya kazi kwa bidii, kutanguliza uzalendo na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuchelewesha kazi na kuuomba Uongozi wa Chico kutafuta betri nyingine za magari ili kazi kuendelea na ujenzi wa mradi huo.

Alisema, mradi huo ni mkubwa na umeletwa kwa manufaa ya mkoa wa Ruvuma kwa hiyo Serikali haitavumilia vitendo vya kiuni kama vilivyofanywa na walinzi wa kampuni ya Hamseki ambao wameacha kutekeleza majukumu yao na kuwa wahujumu wa mradi huo ambao ni muhimu kiuchumi.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa,kampuni ya Chico inafanya kazi kubwa ya ujenzi wa miradi mitatu katika mkoa huo ikiwemo upanuzi wa uwanja wa ndege wa Songea,ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kitai hadi Amani Makolo na barabara ya Mbinga kwenda Wilaya ya Nyasa, inayosubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi.

Aidha amelitaka jeshi la polisi,kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote ya mradi huo ili kampuni hiyo iweze kuendelea na kazi yake.

Awali msimamizi wa mradi huo Wang Jun Yi alisema, tukio hilo ni la pili kutokea ambapo wiki iliyopita watu wasiojulikana walimvamia mlinzi kumjeruhi na kuiba vifaa kwenye moja ya magari ya kampuni hiyo.
Share To:

Post A Comment: