CHAMA cha Waendesha Bodaboda na Bajaj- Taifa kimempongeza Rais John Magufuli kwa namna alivyoshughulikia ugonjwa wa Covid-19 unaoambukizwa na virusi vya corona akiruhusu shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea.

Mwenyekiti wa chama hicho, Edward Mwenyisongola amesema uamuzi huo umekuwa wenye tija kwa waendesha bodaboda na bajaji kwani umewawezesha kuzitumikia familia zao.
Amesema shughuli zisingeruhusiwa kuendelea kama kawaida, wananchi wangekufa kwa njaa huku vitendo vya uhalifu pia vikiongezeka. Amesema waendesha bodaboda wanatoa pongezi na wataendelea kufanya kazi na serikali huku wakitii sheria na kanuni za usalama barabarani.

“Waendesha bodaboda na bajaji tunamshukuru Rais Magufuli na serikali kwa uamuzi wa haki, weledi na uliozingatia maisha ya Watanzania kwa kuruhusu shughuli kuendelea," amesema.
Share To:

Post A Comment: