NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR.

ZOEZI la uchukuaji wa fomu za kutaka kuteuliwa kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) limeendelea tena leo kwa Makada wawili kuchukua fomu.

Wa kwanza kufika alikuwa Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar ambaye aliwahi kuhudumu kuanzia Mwaka 2000-2010, Shamsi Vuai Nahodha aliyefika majira ya saa moja na nusu asubuhi na kisha saa mbili kamili kuingia kusaini na kuchukua fomu.

Baada ya zoezi hilo, Shamsi Vuai Naohodha hakuwa tayari kuzungumza na Wanahabari na baadala yake aliwaomba ushirikiano hapo baadae.

"Nashukuru sana Wanahabari zaidi tuendelee kushirikiana" alisema na kuondoka bila kueleza kwa kina hadhima yake ya kuchukua fomu.

Kada wa pili kujitokeza ni Mtoto wa  aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi Zanzibar, Mohammed  Jafari Jumanne aliyefika majira ya saa tano asubuhi kimyakimya bila wanahabari kumtambua mpaka alipopokelewa na Maafisa wa CCM ndio wakaelezwa kuwa amefika kuchukua fomu

Muhammed Jafari Jumanne naye hakuwa tayari kuzungumza na Waandishi wa Habari zaidi aliwashukuru pekee n kuondoka.

Hadi sasa wagombea hao wanakuwa Saba (7) huku wengine waliokwisha chukua ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk. Hussein Mwinyi aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kwahani Mjini Unguja, Zanzibar, Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Karume, Mbwana Yahaya Mwinyi na Omary Sheha Mussa.

Tukio la kukabdhiwa fomu linatarajiwa kufungwa rasmi 30 Juni huku likisimamiwa na Katibu wa Idara ya Organization CCM, Zanzibar, Cassian Galos.

MWISHO.
Share To:

Post A Comment: