Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta amesema eneo la  wazi la bondeni litatumika kama eneo la kupumzikia wananchi wote wa Arusha.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua eneo hilo lilipo karibu na msikiti wa Bondeni jijini Arusha na kuzungumza na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.
“Eneo hili litatumika kwa ajili ya wananchi kupumzika na haya ni maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli siku aliyotuapisha”.
Aidha,Kimanta amewata waegesha magari wote katika eneo hilo kuondoa magari yao ifikapo Julai Mosi,2020 ili kuliacha eneo hilo wazi kwa ajili ya wananchi kupumzika baada ya shughuli zao za kila siku.
Amesema serikali inampango wa kuliboresha eneo hilo vizuri na kuwa la mapumziko kwa wananchi, kwani eneo hilo linamilikiwa na serikali na ni lawazi.
Pia, amewataka wamiliki wa magari yote yaliyokuwa yameegeshwa katika eneo hilo la wazi kutumia eneo la wazi la Msikiti wa bondeni kuegesha magari yao kwa kufuata taratibu za eneo la Msikiti.
Mheshimiwa Kimanta amefanya ziara fupi katika Jiji la Arusha na kukagua baadhi ya maeneo ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya Terrati.
Share To:

Post A Comment: