Naibu waziri wa TAMISEMI Mhe. Josephat kandege amesema kama Serikali amefarijika na utekelezaji wa mradi wa soko Kibada na kituo cha afya Kigamboni na kuzishauri Halmashauri zingine kuhakikisha zinasimamia vyema miradi ya maendeleo kwa kuzingatia muda na viwango vya miradi kuendana na thamani ya fedha tumika.

Mhe. Kandege amezungumza hayo leo alipotembelea  mradi wa ujenzi wa soko la kisasa linalojengwa Kibada na Uboreshwaji wa kituo cha afya Kigamboni ambapo amesema amefarijika kuona huduma za afya zimeboreshwa  kwa kiwangio kikubwa na maelekezo ya marekebisho aliyoyatoa kipindi cha ujenzi wa majengo mapya ya mama na mtoto yametekelezwa.

Kwa upande wa soko la kibada amesema kukamilika kwa soko hilo kwanza kutasaidia kuondoa adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kuvuka upande wa pili kwenda kufata huduma  na pia Halmashauri  itakua na kitega uchumi ambacho kitaweza  kuongeza mapato.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amemshukuru Naibu waziri kwa kutembelea  miradi na kusema usahuri alioutoa kwenye kituo cha afya Kigamboni  kumewezesha kurahisisha utoaji huduma na kwamba anamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha za uboreshwaji wa huduma za afya ambazo zimewanufaisha wananchi wa Kigamboni.

Mbunge wa Kigamboni Mhe. Faustine Ndungulile ameshukuru Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwekeza Kigamboni na kuwapongeza watendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi na  kutoa rai kuhakikisha wanaendelea kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maendeleo na fedha zinazotolewa na Serikali.

Mkurugenzi wa Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amesema Kigamboni imefarijika sana kwa kupata miradi hususani ya afya kwani  tangu ukamilikaji wa majengo na utoaji wa huduma za mama na mtoto Kituo cha Afya Kigamboni tayari kimeweza kufanya upasuaji kwa wamama 218.

Kwa upande wa soko la kibada Mklurugenzi amesema  hadi ujenzi kukamika kiasi cha Bilioni 6.6 kitatumika  na kwamba Manispaa imejipanga kusimamia mradi ili uweze kukamilka kwa wakati kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi nakuongeza pato kwa Manispaa.
Share To:

Post A Comment: