MRISHO Ngasa, kiungo mkongwe ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kurejea kwenye mechi za ushindani baada ya kuanza mazoezi Mei 27.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.Serikali imeruhusu masuala yamichezo kuanza Juni Mosi na tayari bodi ya ligi imetangaza kuwa Juni 13 ligi itaanza.

Ngassa amesema kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi jambo linalowafanya wazidi kujiamini pale ligi itakapoanza.

“Kila kitu kinakwenda vizuri kwenye mazoezi na kila mchezaji anafurahi kwani tulikuwa nje kwa muda mrefu, kwa sasa tupo tayari kurejea uwanjani ili kuendelea pale ambapo tuliishia,” amesema.
Yanga ikiwa imefunga mabao 31, Ngasa amehusika kwenye mabao matatu, akifunga mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Share To:

Post A Comment: