Na Woinde Shizza  , .MONDULI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Idd Kimanta, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Monduli  ACP Edward Balele kuwa Wilaya ya Monduli haijawai kupata hati chafu tokea serikali ya awamu ya tano iingie madarakani hivyo na kumtaka aendelee kusimamia vyema ili hati chafu usiwepo..
Mheshimiwa Kimanta ameyasema hayo juzi alipokuwa akimkabidhi ofisi Mkuu huyo wa Wilaya katika ofisi za wilaya ya Monduli na kisha kuzungumza na watumishi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya na halmashauri.

Amemtaka Mkuu uyo wa Wilaya kuhakikisha hadhi ya Wilaya ya Monduli inabaki kama ilivyo.
“Nakukabidhi Wilaya hii ya Monduli na watumishi wote wakiwa katika hali nzuri na wewe hakikisha unaendelea kufanya nao kazi vizuri na kwa ushirikiano mkubwa”.
Amesema watumishi wa Monduli kwa ujumla ndio waliofanikisha mafanikio yake hadi kufikia nafasi hiyo ya mkuu wa Mkoa, hivyo amewashukuru kwa ushirikiano wao waliouwonesha na kuwataka waendelee hivyo hivyo hata kwa mkuu huyu mpya wa wilaya.

Amesema Kimata ameacha alama kubwa na nzuri sana katika wilaya hiyo na kuaidi kuyaendeleza yale waliyoweza kujifunza kutoka kwake huku wakishirikiana na Mkuu mpya wa wilaya.
Mheshimiwa Kimanta amekabidhi ofisi yake ya zamani ya wilaya kwa mkuu mpya wa wilaya hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema wiki hii.
Akizungumza Mara baada  ya kukabithiwa ofisi ACP Edward Balele aliahidi kumpa ushirikiano Mkuu wa mkoa Arusha na pia Kuwapa ushirikiano watumishi wa idara zote.

Mkuu wa wilaya amenza kazi Mara Moja kwa Kuendelea kusikiliza Wananchi na kutatua changamoto zao wanaofika ofisini kwake sanjari nahilo  Pia amefanya ziara ndogo kwa kutembea Kituo cha Polisi Monduli na kuzungumza na maafisa wa polisi.
 
 Wakati huo huo Dc Balele amdhamini Mgombea Uraisi Mheshimiwa Raisi John Pombe Joseph Magufuli mara baada kufika Ofisi za Chama Wilaya ya Monduli kwa mara kwanza.
Share To:

Post A Comment: