Wednesday, 24 June 2020

HOSPITALI YA CCBRT YATEMBELEWA NA MAAFISA WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

HOSPITALI ya CCBRT wametembelewa na Maafisa kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini, kwa lengo la kujionea kazi zinazofanywa na CCBRT. 

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi, aliwapitisha katika maeneo kadha na vitengo tofauti katika hospitalini hiyo ili kujionea namna wanavyofanya kazi na kuwahudumia watanzania.

Hata hivyo Maafisa kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini wamefurahishwa na kazi tunazozifanywa  na hospitali hiyo katika kutimiza wajibu wao kwa kutoa huduma kwa wanzania.

 "Siku zote tunajivunia kuwa na wadau wa aina hii, wanaotutembelea  hospitali yetu katika maeneo mengine tunayofanya kazi kwa ajili ya kutuunga mkono katika kutoa huduma." Wamesema Maafisa kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini.

Licha ya hilo hospitali ya CCBRT wameshauriwa kuboresha zaidi na zaidi kwa kile wanachokifanya katika jamii ya watanzania.
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akizungumza na Maafisa kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini walipotembelea hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo.
  

  Mazungumzo yakiendelea wakati wakitembelea hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment