Na Esther macha, Mbeya

BAADA ya kuhitimisha kikao cha mwisho cha baraza la madiwani wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, Diwani wa Kata ya Luhanga kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHadema) Dira Funika amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu wa Chama cha mapinduzi wilayani Mbarali, Abdullah Mpokwa alisema diwani huyo hajashawishiwa na mtu yeyote amerudi kwa hiyari yake mwenyewe.

Kwa upande wake Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Luhanga (Chadema) Dira Funika alisema kuwa ameamua kurudi nyumbani kwani toka mwanzo amelelewa na chama cha mapinduzi .

Dira alisema kuwa ni makosa machache Sana ambayo yalifanywa na viongozi wa ccm ambayo yalipelekea kuhamia kwa mama kambo.

"Hivi sasa nipo tayari kuwatumikia wanachama wote wa chama cha mapinduzi, nimerudi nyumbani mwenyewe kwa hiyari yangu "alisema aliyekuwa Diwani wa Chadema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbarali, Hashim Mwalyawa alisema kitendo cha Diwani huyo kurudi chama cha mapunduzi kimemfurahisha Sana na anaamini kuwa watakuwa pamoja kukijenga chama hicho.

Mwisho.
Share To:

Post A Comment: