Wednesday, 13 May 2020

UWASWATA WASAIDIA SERIKALI KUPAMBANA NA CORONA


NA HERI SHAABAN
UMOJA wa Wazalishaji Sabuni wadogo Tanzania (UWASWATA) wamechangia SERIKALI ya Mkoa Dar es Salaam, sabuni lita mia nne hamsini kwa ajili ya kujikinga na janga la COVID 19 corona .

Sabuni hizo zimepokelewa na Ofisa  Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasirimali Watu Lawrence Malangwa

Akizungumza wakati wa kukabidhi Sabuni hizo Katibu wa Umoja huo wa UWASWATA Maria Lucas alisema  umoja wao wa UWASWATA umeguswa wamelazimika kuungana na juhudi za serikali katika kupambana na janga ili.

"Umoja huu uliundwa chini ya ofisi ya Mkemia Mkuu na SIDO ndio walezi wetu ambapo mpaka sasa jumla ya wanachama mia wa Umoja huu" alisema Maria .


Maria alisema misaada hiyo wanaendelea kuisaidia serikali ni endelevu hatua kwa hatua dhumuni kusaidia jamii na kutoa elimu kuhusiana na ugonjwa huo wa covid 19 corona.


Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa juhudi zake kubwa anazochukua katika kupambana na kutokomeza covid 19 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwaupande wake Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasirimali Watu Lawrence Malangwa alisema sabuni zitapelekwa maeneo muhimu ili kusaidia jamii   katika mapambano ya Corona.

Malangwa aliwataka wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kujitokeza kusaidia Serikali  katika mapambano hayo .

Naye Mkufunzi na sabuni na  vipodozi SIDO  Mkoa Dar es Salaam George Buchafwe aliwataka wafanyabiashara na Wajasiriamali kujiunga na SIDO katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli ili kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda .

George alisema nchi yetu inapokuwa na viwanda vingi uchumi pia unakuwa na upatikanaji wa masoko unaongezeka .

Mwisho

No comments:

Post a Comment