Waumini Marafiki wa Mtakatifu Rita wa Kashia, Kanisa  Katoliki Jimbo la Singida wakiwa kwenye maombi ya Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwenye Kituo cha Hija kwa Bikira Maria kilichopo Kijiji cha Sukamahela WIlaya ya Manyoni mkoani hapa jana, kwa namna anavyoendelea kulilinda Taifa dhidi ya ugonjwa wa Corona.
 Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (mbele) Aliyemuakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Dkt.Rehema Nchimbi akiongoza Waumini  kwenye maombi hayo.
 Maombi yakifanyika mbele ya Sanamu ya Bikira Maria.
 Waumini wakiandamana kuelekea kwenye maombi hayo.
 Maombi yakiendelea.
 Ndahani akiongoza tafakari  wakati wa maombi hayo.
 Mwenyekiti wa WAWATA Jimbo Katoliki la Singida, Veronica Mwambuta akiongoza sala maalumu ya shukurani.
 Sister Maria Subi akizungumza wakati wa maombi hayo.
 Maombi yakiendelea.
 Mwakilishi wa Wanavyuo mbalimbali waliopo ndani ,ya Mkoa wa Singida kutoka Chuo cha St Joseph Dar es Salaam, Lucas Stephano akitoa ombi maalumu dhidi ya Corona.
 Maombi yakiendelea.
 Muonekano la eneo la Hija la Sukamahela.
 Mandhari ya eneo hilo.
Ujenzi wa Kanisa lililopo katika kituo hicho cha Hija ukiendelea.



Na Godwin Myovela, Singida

Na Godwin Myovela, Singida

KAIMU Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida, Mwalimu Frederick Ndahani ameongoza waumini wa Kanisa Katoliki ambao ni marafiki wakubwa wa Mtakatifu ‘Rita wa Kashia’ mkoani hapa kwenye maombi maalumu ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea kuwalinda na kuwaepusha watanzania dhidi ya madhara yatokanayo na janga la Covid- 19
Ndahani, ambaye alimwakilisha Mkuu wa , Dkt. Rehema Nchimbi kwenye kusanyiko la maombi hayo yaliyofanyika jana eneo la Sukamahela, wilaya ya Manyoni mkoani hapa, linalosadikiwa kuwa kati kati ya Tanzania, eneo ambalo Kanisa Katoliki limejenga kituo cha hija kwa heshima ya Bikira Maria
“Tumekuja hapa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea kulipigania taifa letu kupitia maombezi ya Bikira Maria dhidi ya janga la corona. Na tumeamua kufanya maombi yetu eneo hili kwa sababu lipo katikati ya nchi na ndio kitovu…lakini zaidi mama huyu yupo hapa na kwa maombezi yake anaendelea kuimarisha ulinzi wa taifa letu,” alisema Ndahani
Ndahani ambaye ni miongoni mwa vijana walioshiriki kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2017, katika hotuba yake amemfananisha Rais John Magufuli na Nabii Musa kwa namna anavyoongoza taifa kwa unyenyekevu na maono ya kimungu huku nchi ikishuhudia miujiza mikubwa katika kipindi hiki kigumu.
Kijana huyo ambaye amekuwa na juhudi kubwa za kuhamasisha umoja wa kitaifa kupitia vijana wa mkoa wote wa Singida, amewataka watanzania walionusurika na ugonjwa wa Corona na wale waliopona kuendelea kuchukua tahadhari zinazoelekezwa na wataalamu na Rais, ili kuepuka maambukizi mapya.
“Kwa wakristu mkifatilia kitabu kile cha ‘Kutoka’ mtakumbuka namna Mungu alivyomuongoza Musa katika kuwavusha wana wa Israeli kwenye bahari ya Shamu kwa kutumia ile fimbo…na ndivyo baba yetu Magufuli anachokifanya kwa sasa,” alisema Ndahani huku akishangiliwa
Kupitia maombi hayo ya shukrani, Sista wa Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Katoliki la Singida, Maria Subi, alisema anamshukuru Mungu kwa namna ya kipekee hasa anavyojidhihirisha katikati ya kiongozi mkuu wa Tanzania Rais Magufuli, kwa namna anavyoonesha hekima na utulivu mkubwa... wakati wote anaposhughulikia suala la corona
“Kwa nguvu yake Mwenyezi Mungu furaha na amani ya watanzania imeanza kurejea tena, na tayari tumeanza kuungana na wageni mbalimbali kwa kuwakaribisha. Naamini sasa tutaendelea kufanya kazi zetu kama kawaida na nchi itachangamka kama mwanzo, tunapaswa kumshukuru Mungu” alisema Subi. 
Share To:

Post A Comment: