Halmashauri ya Wilaya ya Meru imepata Hati Safi kwenye ukaguzi wa hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Hati hiyo safi imepatikana kufuatia barua iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,

Akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Mhe. Will J.  Njau amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Emmanuel Mkongo kwa usimamizi mzuri wa fedha za umma na kupelekea Halmashauri hiyo kupata hati safi.     

 Aidha, Mhe. Njau amewapongeza pia Wakuu wa Idara na Vitengo,  Watumishi na Waheshimiwa  Madiwani  kwa kutekeleza wajibu wao na kuwezesha Halmashauri hiyo kufanya vizuri.

Naye Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Meru, Emmanuel Mkongo  amesema siri ya kupata hati safi ni  matumizi ya fedha yanayozingatia Sheria,  Kanuni, Taratibu na Miongozo  ya fedha za Umma pamoja na Watumishi kuzingatia weledi, uadilifu na maadili ya Utumishi wa Umma.

Mkongo amesema kuwa, Halmashauri inamkakati wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha inaendelea kupata hati safi.

Mkongo ametoa hongera  kwa watumishi wote  na kuwataka wachape kazi kwa kuzingatia weledi, uwajibikaji na uadilifu kwa kuweka mbele uzalendo na maslahi mapana ya Umma na Taifa kwa ujumla.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: