Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mwenyekiti wa Madereva stand ya Daladala Kilombero vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona huku akifuatiliwa na Meneja msaidizi wa Tanalec Michael Mangowi Leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Sehemu ya msaada uliotolewa na Tanelec Ltd ikiwemo Ndoo 100 za maji Tiririka na Sabuni katoni 100 ikiwa ni kwa ajili ya Mapambano dhidi Ugonjwa wa Covid 19 leo jijini Arusha.

Vifaa vilivyotolewa leo na Tanelec Ltd kwa Serikali ya mkoa wa Arusha ikiwa ni kusaidia kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona

Sehemu ya wadau walioshiriki hafla hiyo leo iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini hapa.

Wadau wakifuatilia hotuba ya kumshukuru ilivyokuwa imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo

Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Arusha wakifuatilia taarifa ilivyokuwa ikitolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega hayupo pichani leo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akitoa taarifa ya hali ya Ugonjwa wa Covid 19 kwa mkoa wa Arusha na hatua ambazo Serikali imeendelea kuchukuwa kuhakikisha inatoa elimu na vifaa kwa ajili ya kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19

Meneja msaidizi wa Tanelec Ltd Michael Mangowi akieleza mbele ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo vifaa walivyochangia kwa ajili ya kukabiliana na Ugonjwa wa Covid 19 leo jijini Arusha kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

Katibu wa Daladala mkoa wa Arusha Said Shariff akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo jijini Arusha

Mwenyekiti wa Mtaa wa Levolosi Seif Abdi akipokea vifaa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo

Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Arusha Locken Adolf akiwa na Mwenyekiti wa Akiboa wakipokea vifaa hivyo vya kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19 kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha


Vifaa vikiendelea kutolewa Leo na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo hii ikiwa ni vifaa kwa ajili ya Soko kuu kwa niaba yao na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara mkoa wa Arusha Locken Adolf leo jijini Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiongea Mara baada ya kutoa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwenye maeneo ya Stand masoko na vituo vya Polisi 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea Msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 kutoka kwa Meneja msaidizi wa Tanelec Ltd Michael Mangowi huku akifuatiliwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega leo kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Waandishi wa Habari Dotto Kadoshi ETv Veronica Mheta Habari leo Asraji Mvungi ITV Emanuel Sauli wa Triple A Fm akipokea Msaada wa lita 40 ya vitakasa mikono kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa niaba ya waandishi waliokuwa kwenye tukio hilo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Covid 19 leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Jeshi la Polisi kwa niaba ya Kaimu kamanda wa mkoa wa Arusha Koka Moita wakipokea vifaa ikiwa ni kwa ajili ya vituo vya polisi kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona leo Jijini Arusha.

Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Arusha Haniu Haniu akipokea vifaa vya kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa mkuu wa mkoa vilivyotolewa na kampuni ya Tanalec Ltd ya mkoa hapa leo Leo kwenye Ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.


Ahmed Mahmoud Arusha
Tanelec imeanza kufanya utafiti wa mashine za kusaidia wagonjwa kupumulia kwa mashine katika kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 na magonjwa mengine.
Akiongea Meneja msaidizi wa Tanalec Michael Mangowi kwenye hafla fupi ya makabidhiano kwa serikali mkoa wa Arusha  ya vifaa vya kutakasa mikono ambazo ni sabuni  100 sanjari na ndoo 100  kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Covid 19.
Alibainisha kuwa taasisi hiyo kupitia wafanyakazi wake imeendelea na utafiti wa kutengeneza mashine hizo pamoja na mashine nyengine ya kupita na kumwagiwa dawa ya kutakasa mwili mzima kwa lengo la kuendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa covid 19.
“Tumejipanga kuhakikisha tunaendelea na utafiti wa kuhakikisha tunapambana na ugonjwa wa Covid 19 kusaidia vitakasa mikono na mwili ili kuweza kuisaidia serikali yetu dhidi ya janga la ugonjwa wa covid 19”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alishukuru kwa msaada huo kwa kuwa ugonjwa huo hauchagui viongozi wala mtu yoyote
Alisisistiza kuwa Mkoa wa Arusha umejidhatiti katika kuimarisha udhibiti wa wahamiaji haramu wanaoingia  maeneo ya mipaka haswa mpaka wa Namanga uliopo Wilayani Longido pamoja na mpaka wa Ngorongoro uliopo wilayani Ngororongoro unaopakana na nchi jirani ya Kenya
Alisisitiza kuwa kunabaadhi ya watu wameshakamatwa kuhusiana na kupita katika mipaka kwa njia za kinyemela na kuziomba taasisi ,mashirika na watu mbalimbali kujitokeza kwaajili ya kuchangia vitu mbalimbali ili kudhibiti ugonjwa huu wa Corona.
Naye mmoja kati ya wanufaika na  msaada huo wa kujikinga na Corona ,Mwenyekiti wa Stendi Kuu ya Mabasi Maulid Rajabu  alishukuru kwa msaada huo na kusisitiza kuwa hivi sasa wanajitahidi kutoa elimu juu ya ugonjwa huo sambamba na kuhakikisha kila basi linakuwa na ndoo pamoja  na sabuni kwaajili ya kunawia mikono.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: