SERIKALI YAOMBWA KUTAFUTA NJIA MBADALA KUVIFIKIA VIJIJI VISIVYOFIKIKA ILI KUVIPATIA ELIMU JUU YA COVID-19


Serikali imeombwa kuhakikisha kwamba inatafuta njia mbadala ,kwaajili ya kuwafikia wananchi waliopo maeneo ambayo hayafikiki kiurahisi, kwaajili ya kuwapatia elimu ya kuepukana maambukizi ya homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya Corona  (COVID-19

Hayo yamesemwa na Mchungaji  David Chikawe Katibu wa Kanisa la Mission to Unreaches Area nchini (MUAC),lililopo Kibaha mkoa wa Pwani na kusema kuwa asilimia kubwa wananchi waliopo vijiji visivyofikiwa kiurahisi hawana uelewa juu ya ugonjwa huu

‘’Ni ukweli kwamba tunaendelea na ibada ila tumezingatuia ushauri wa serikali, wa watu kufanya usafi kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, hivyo kwenye nyumba za ibada zote za MUAC tumeweka maji na sabuni katika kila ofisi za kanisa, watu wanapoingia lazima wanawe mikono’’Alisema Mch.David

Amesema kanisa hilo limeweka utaratibu ambao utawasaidia waumini wao,kwa kupitia  viongozi wa kanda kwa kutengeneza kundi la mtandao wa kijamii ( Whatsap)ambalo linawaunganisha na wanawasiliana kila mara,ili kutoa elimu na taarifa na kwa waumuni hao namna ya kuchukua tahadhari juu ya COVID-19, sambamba na kutokuwa na msongamano wakati wa ibada

‘’Kuna watu wengine wapo mbali sana ,siyo rahisi sisi kuwapata ,ila tunawatumia hawa viongozi wa Kanisa kanda ili kuwapata ,kwasababu wananzo namba za wachungaji wa maeneo husika, hivyo inakuwa rahisi kumpatia taarifa zilizopo juu ya ugonjwa huu wa Corona ili na yeye aweze kufikisha kwa waumini huko walipo namna ya kujikinga’’

Amesema kwa njia hiyo ya mtandao inasaidia kwa kiasi kidogo ,bado elimu inahitajika katika maeneo mengi yasiyofikiwa, amesema tatizo hilo ni kubwa na linahitaji kuwa na tahadhari kubwa ,kuanzia ngazi ya kaya,vitongoji  hadi Taifa kwa ujumla

‘’Yapo maeneo ambayo hayawezi kufikika aidha kwa gari ,pikipiki wakati mwingine ,ila ninachojua serikali inamkono mrefu inaweza kufanya mambo mengi hata kuweza kuwafikia watu kule walipo, kwani simu tunazozipata inaonyesha bado watu wengi hawana elimu juu ya janga hili’’.alisema Mch.David

Aidha Kanisa hilo la MUAC, limepongeza hatua ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli, kutangaza siku tatu kwaajili ya maombi kwa Taifa ambapo wamesema wameunga mkono kwa asilimia 100% ,amesema kabla ya tangazo la Rais tayari walishaanza maombi ya wiki nzima,, hivyo wameendelea kuunga mkono kuomba kwani wazo hilo sahihi na limekuja  kwa wakati sahihi  

Aidha alisema hajasikia nchi yeyote Rais ametangaza tangazo kama hilo, hivyo ameasema Rais Magufuli amefanya jambo zuri la busara ,ambalo linaweza kuonekana  kwa viongozi wa awali katika Maandiko Matakatifu,waliweza kufanya maamuzi yalipokuwa akitokea majanga, waliweza kuwatangazia watu wao namna ya kumrudia Mungu, kwa kufunga na kuomba toba.

‘’Sijasikia nchi yeyote Rais anatangaza tangazo kama hili, kwahiyo kusema ukweli Dr.Magufuli  amefanya kitu kizuri cha busara ,ambacho tunaweza kukiona hata kwa viongozi mbalimbali katika Biblia, ambapo walifanya maamuzi alipokuwa yanatokea majanga, waliweza kuwatangazia watu wao’’ Alisema

Hivyo amewasihi Watanzania kuungana kwenye maombi, huku akiwataka wale wanaoweza kufunga wafanye hivyo,na wale wasioweza wasiache kuomba ili kuungana na Rais wa Nchi

Aidha ametoa wito kwa jamii kwamba watambue kuwa kila mwanadamu anapaswa kujiuliza kwani  matukio kama haya kwa wasomaji wa biblia yalishawahi kutokea na ipo miji,nchi  zilifutwa na majanga huku akitolea mfano Sodom na Gomora ambao waliteketezwa kwa moto,pia Mfalme wa Israel Daudi alimkosea Mungu  na Taifa lake likapata mapigo

‘’Siwezi kusema kwamba ni Mungu anaichapa dunia, ila ninachoweza kusema kwa ujasiri ni kwamba Mungu alifahamu, na ameruhusu ili kuwafanya wanadamu wajue kwamba kwa nguvu zao wenyewe hawawezi, kwahiyo wanamuhitaji Mungu,hivyo mwitikio wa dunia nzima watu wanamtafuta Mungu’’ Alisema

Hivyo ametoa rai kwa jamii watambue kwamba wakati huu ni  wa kumrudia Mungu, maana yupo na wanadamu wanadhiirisha hawawezi  peke yeo kwa nguvu zao wenyewe ,amesema gonjwa hilo limekuja kudhihirisha kuwa pamoja na teknolojia zilizopo,elimu,na vyote walivyonavyo wanadamu haviwezi bali wanamuhitaji Mungu pia inadhihirisha kuwa Mungu anavunja kiburi cha mwanadamu

Nashauri mtu yeyote asiwe na kiburi,jeuri aache anayoweza kuyafanya na amrudie Mungu, kama anaona sivyo basi aendelee kukaa mtaani, na kufanya anayofanya lakini atakuja kujua baadae kwamba alichezea muda wake. alisema Mch David

Mchungaji Ch ikawe amesema muda walionao siyo muda wa kufanya mambo ya hovyo, badala yake wautumie muda wa kutulia ikwezekana na kutulia na familia,wajaribu kumtafuta Mungu, kumuomba ili aliepushe Taifa na janga hilo la Covid-19

Aidha Kanisa hilo la Mission to Unreached Area (MUAC) lenye makao yake makuu nchini Tanzania katika wilaya ya Kibaha mkoni Pwani lina jumla ya makanisa 400 ambapo nchi ya  Kenya yapo makanisa zaidi ya 10 na Congo yapo makanisa 3 ambapo makanisa mengi ya huduma hiyo yapo nchini ambapo kwa asilimia kubwa yapo vijijini siyo mijijini

MWISHO

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: