Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiwakataza watu wanaotumia sabuni ya maji au ya unga kuchanganya na maji jambo ambalo amedai linapunguza ubora wa sabuni hizo juu ya kupambana na wadudu

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kufuata maelekezo ya Serikali juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virusi vya Covad 19.mwandishi Amon Mtega anaripoti toka Songea 

Mndeme ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wamiliki wa magari ya abiria wa Manispaa  ya Songea juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Mkuu huyo ambaye amepita kukagua tahadhari zinazochukuliwa na wafanyabiashara hao katika maeneo yao ya biashara ikiwemo eneo la Soko kuu la Songea ,Mazese na Stendi  kuu ya daladala mjini humo, amesema kuwa kama kilammoja atachukua tahadhari juu ya ugonjwa huo  itakuwa ni rahisi kutoweka kwa ugonjwa huo.
Katika hatua nyingine mkuu huyo aliwageukia watu ambao wanajifanya hawataki kutumia vitakasa mikono yaani kunawa maji pindi wanapoingia katika maeneo mbalimbali ya huduma kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwalaza lumande.
  Amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanajifanya ni wababe hawataki kutumia vitakasa mikono ikiwemo kunawa maji kwa sabuni jambo ambalo halitavumiliwa.
Hata hivyo amewataka madereva daladala na waendesha bodaboda kuacha tabia ya kuzidisha abiria kwenye vyombo hivyo ,maana kuzidisha abiria ni kosa la kisheria na linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo wa corona.
Pia amewataka watu wanaoweka vitakasa mikono katika maeneo yao ya kazi ikiwemo ndoo za maji kuacha tabia ya kuviharibu vitakasa mikono hivyo yaani sabuni za maji au za unga kuacha kuzi zimua na maji.
                 MWISHO.
    

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: