Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitoa taarifa ya shughuli mbalimbali zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha kati ya January na Aprili mwaka huu.
 Taarifa ikitolewa kwa waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Mkuu wa PCCB Wilaya ya Manyoni, Jerome Mpanda, Naibu  Mkuu wa PCCB Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege,  Mkuu wa PCCB Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda na  Mkuu wa PCCB Wilaya ya Mkalama, Yassin Mohamed.
 
 Mkutano na waandishi ukiendelea. Kutoka kushoto ni Naibu  Mkuu wa PCCB Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege, Mkuu wa PCCB Wilaya ya Manyoni, Jerome Mpanda na Mkuu wa PCCB Wilaya ya Manyoni, Jerome Mpanda na Mkuu wa PCCB Wilaya ya Ikungi,  aliyejitambulisha kwa jina moja la Nyoni.
 Maofisa wa PCCB wakiwa katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkutano ukiendelea.
Jengo la Ofisi ya PCCB Mkoa wa Singida.
Na Dotto Mwaibale, Singida

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) inawashikilia Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani hapa, Albert Ngimba na mwenzake mmoja kwa makosa ya kushawishi na kutoa hongo ya shilingi laki tano kwa afisa uchunguzi wa Takukuru.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana kwenye ofisi  za PCCB, Mkuu wa Takukuru mkoa wa Singida, Adili Elinipenda, alisema azma hasa ya watuhumiwa hao kutenda kosa hilo ilikuwa ni kumshawishi afisa huyo wa Takukuru  awasaidie kwenye uchunguzi unaohusiana na tuhuma za ufujaji na ubadhirifu wa fedha zilizotolewa na Serikali Kuu.
Elinipenda alimtaja mtuhumiwa mwingine wa sakata hilo kuwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Isenengwa wilayani humo, George Mmembwa ambao kwa pamoja walishiriki katika ufujaii wa fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya nyumba za walimu na vyoo .
“Watuhumiwa hawa walikamatwa juzi majira ya saa nne usiku nyumbani kwa afisa huyo wa Takukuru wakiwa wamempelekea kiasi hicho cha pesa (shilingi laki tano) kama sehemu ya shilingi milioni nne waliyokuwa wamemuahidi,” alisema Elinipenda.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea na kwamba utakapokamilika watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.
“Takukuru mkoa wa Singida inatoa wito kwa wananchi kuongeza kasi ya ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa, lakini pia kujitokeza mahakamani pindi wanapohitajika kutoa ushahidi wao,” alisema Elinipenda.
Aidha, katika hatua nyingine katika kipindi cha Januari na Aprili mwaka huu, ofisi ya Takukuru mkoani hapa imewapandisha kizimbani watuhumiwa wapatao 13 wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za vitendo vya rushwa.
“Kuna kesi 6 zenye jumla ya watuhumiwa 13 zilifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashauri ya jinai, na kati ya kesi hizo tatu zilitolewa hukumu na kushinda,” alisema na kuongeza;
“Vilevile  katika kipindi husika Takukuru mkoani hapa ilifanya operesheni maalum ya kufuatilia Vyama vya Ushirika, kupitia zoezi hili jumla ya fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni arobaini na nane (48,906,938) ziliokolewa,” alisema Elinipenda.                                                  
Share To:

msumbanews

Post A Comment: