Friday, 13 March 2020

WAZIRI UMMY KUFUNGUA MKUTANO WA WAFAMASIA -

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST), utakaombatana na Kongamano la Kisayansi.
-
Rais wa Chama Cha Wafamasia (PST), Issa Hango amesema hayo leo Machi 13, alipozungumza na waandishi wa habari kwamba mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Kisenga, LALF Kijitonyama Machi 16 na 17, mwaka huu.
-
"Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Wafamasia Tanzania Wadhamiria Kuongoza Mpango Mkakati wa Kukuza Viwanda vya Dawa Nchini Tanzania," amesema.
-
Amesema katika mkutano huo, wanataaluma wa kada ya famasi nchini watatoka na maazimio ya namna bora ya kushiriki kikamilifu katika eneo la viwanda vya dawa nchini kama njia sahihi ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye usalama na ufanisi.
-
Amesema katika kongamano hilo pia wataweka bayana mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano ikiendana na uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu kama vile hospitali na zahanati.
-
Ameongeza "Kwa upande wetu (wafamasia), tutazungumzia hasa eneo letu la upatikanaji wa dawa kutokana na ongezeko kubwa la bajeti ya dawa, kutoka Sh. Bil 31 mwaka 2015 hadi Sh. Bil 267 kufikia sasa.
-
"Nitoe rai kwa wanataaluma wetu kufika kwa wingi kuhudhuria kongamano hili muhimu,"

No comments:

Post a comment