Thursday, 12 March 2020

WAFANYABIASHARA JIJINI MBEYA WATAKIWA KUJENGA URAFIKI NA TRA


 Afisa huduma kwa mlipa kodi wa TRA Emmanuel Msambwa akitoa elimu kwamfanyabiashara.
...............................................
Na Esther Macha, Mbeya

WAFANYABIASHARA Jijini Mbeya wametakiwa kuwaona maofisa wa TRA kama marafiki kutokana na kuwa wanakusanya mapato ambayo yanaisaidia serikali kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kama kujenga barabara, kununua dawa za hospitali na vifaa tiba.

 Justone Luvanda ni mfanyabiashara wa Kasumulu wilayani Kyela alisema kuwa ipo haja kwa wafanyabiashara kutojenga chuki na maafisa wa mamlaka ya mapato TRA.

"Mimi nitoe tu wito kwa wafanyabiashara wenzangu hapa mpakani na sehemu nyingine kuwa tuwape ushirikiano maofisa wa TRA kwa kuwa wanakusanya mapato ya serikali ambayo yanatuwezesha kupata huduma za kijamii na kuboresha miundo mbinu mbalimbali inayochochea maendeleo", alisema Luvanda.


TRA inaendesha kampeni maalumu ya kutoa elimu kwa Mlipakodi mkoa kwa mkoa na sasa ipo mkoani Mbeya na Wilaya zake kuhakikisha elimu ya Kodi inawafikia wafanyabiashara na wananchi wote.

 Rose Nelson ambaye ni mmiliki wa duka la bidhaa za jumla mpakani Kasumulu  ameishukuru TRA kwa kuanzisha kampeni ya elimu kwa Mlipakodi na kuongeza kuwa itawasaidia wafanyabiashara wa mipakani ambao wamekuwa na uelewa mdogo wa masuala ya ulipaji kodi na kwamba ingekuwa rahisi kwa wao kupotoshwa kwa kupewa taarifa zisizo sahihi na watu wa mtaani.

Nelson alisema kuwa kampeni iliyoanzishwa ya TRA ni nzuri kwani baadhi ya wafanyabiashara wataanza kupata uelewa juu yas muhimu wa kulipa kodi ambayo ni kwa ajili ya maendeleo.

No comments:

Post a comment