Monday, 2 March 2020

TANZANIA YATAJWA NCHI YA 21 DUNIANI YA NNE AFRIKA NA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KWA KIWANGO CHA BIASHARA NDOGONDOGO NA UBORESHAJI NA KUANDAA WAFABIASHARA WADOGO WADOGO MACHINGA

Msemaji mkuu wa Serikali na Katibu mkuu wa wizara ya habari Sanaa Michezo na utamaduni Dkt Hassan Abass akiongea na vyombo vya habari 


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Tanzania yatajwa kuwa nchi ya 21 Duniani ,ya 4,Afrika na ya kwanza
Afrika Mashariki  kwa kiwango cha biashara ndogondogo na Uboreshaji wa
Machinga.
Hayo yamesemwa leo Machi,1,2020 jijini Dodoma na Msemaji mkuu wa
Serikali Dkt.Hassan Abbasi  wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari
ambapo amesema hatua hiyo inatokana na jitihada kubwa zinazofanywa na
serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Dkt. Abbasi  ambaye pia ni katibu Mkuu ,Wizara ya Habari,Utamaduni
,Sanaa na Michezo pamoja na Mkurugenzi mkuu   Idara ya Habari Maelezo
amesema hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya  RMB Where to Invest In Africa
ya Mwaka 2020 ambapo nchi ya kwanza Afrika kwa kiwango cha biashara
ndogondogo na uboreshaji wa machinga ni Morocco,ya pili ni Algeria,ya
tatu ni Ivory Coast ,ya nne ni Tanzania  zikifuatiwa na Kenya,Afrika
Kusini na Nigeria.
Kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa[SGR]  Dkt. Abbasi amesema Kipande cha
Dar Es Salaam hadi Morogoro hadi sasa umefikia asilimia 75% huku
Morogoro mpaka Makutupora ya Singida ukifikia zaidi ya asilimia 28%
ikijumuisha uwekaji wa nguzo na nyaya za umeme ambapo Fedha
zilizotumika hadi sasa ni Trioni 2.957 huku tenda ya ujenzi wa reli ya
Kisasa  [SGR] ya Mwanza-Isaka  mpaka Rwanda na Burundi kutangazwa muda
wowote kuanzia sasa.
Pia,Dkt.Abbasi amesema kesho Tarehe,2,Machi,2020 Makatibu wakuu wote
wa Wizara watatembelea mradi wa ujenzi wa reli ya Umeme .
Katika Mradi wa kufua Umeme wa  Rufiji ujulikanao kama [Julius
Nyerere]ambao una hatua tatu, kwenye kuchoronga handaki la kupitisha
maji ya mto [excavation of tunnel] imekamilika kwa asilimia
100%,kuweka zege la kuimarisha handaki [reinforcement and concrete
lining of tunnel] imefikia asilimia 10% ya ujenzi na hadi kufikia
Januari ,2020 zimetumika Trilioni 1.275 katika utekelezaji wa mradi
huo.
Kuhusu Chelezo  Dkt.Abbasi  amesema imekamilika na inasubiriwa
kujaribiwa tarehe 16,Machi,2020 kwa uzito uliosanifiwa  tani elfu
nne[4000] na zimelipwa  Dola Milioni 14.2 kati ya Dola milioni 15.8
sawa na asilimia 90% ya malipo ,Fedha hizo ni sawa na Tsh.Bilioni
32.8.
Katika ujenzi wa Meli ya Mv Viktoria  Dkt.Abbasi amesema umefikia
asilimia 89% na hadi sasa zimelipwa Tsh.Bilioni 14.2 kati ya
Tsh.Bilioni 22.7% za kwenye mkataba sawa na asilimia 63%.
Aidha,Dkt.Abbasi amefafanua kuwa ,Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya
Afrika [AfDB] ya Mwaka 2020 imeitaja Tanzania kuwa nchi yenye mageuzi
yanayogusa na kubadili maisha ya watu na iliyopiga hatua kupunguza
umasikini huku pia shirika la Habari la kimataifa la CNBC Africa
tarehe 29,Februari,2020 limerusha kwa zaidi ya nchi 100 duniani makala
inayoelezea Mafanikio ya Tanzania katika sekta mbalimbali
iitwayo”Tanzania ,the Soul of New Africa.

No comments:

Post a comment