Mrajisi Msaidizi anayesimamia vyama vya ushirika wa Kifedha kutoka Dodoma Josephat Kisamalala akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
 AFISA Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dodoma Boniphace Moshi akizungumza wakati mafunzo hayo
 MRAJISI Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jackline Senzige akizungumza wakati wa mafunzo hayo
 Sehemu ya washiriki kwenye mafunzo hayo


 Sehemu ya washiriki kwenye kikao hicho wakifuatilia matukio mbalimbali


VYAMA vya Ushirika wa Akiba na Mikopo nchini (Saccos) vimetakiwa kuweka nguvu kubwa kwenye uwekezaji kwa kutoa mikopo kwa wanachama wao kwa asilimia 70 hadi 80 viwekezwe huku ili viweze kupata ufanisi mkubwa na wenye tija.

Hayo yalisemwa na Afisa Ushirika wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dodoma Boniphace Moshi wakati wa mafunzo kwa viongozi wa Saccos Mkoani Tanga yanayohusiana na usimamizi wa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo kwa kuzingatia sheria ya ushirika namba 6 ya mwaka 2013 ambapo kiwango hicho kinatokana na mali ambazo wameziweka.

Moshi alieleza hayo wakati akiwasilisha mada ya Sera ya Uhasibu na Fedha wakati wa mafunzo hayo ambapo pia alisema hiyo ni sheria namba 10 ya mwaka 2018 pamoja na kanuni zinazo simamia sekta ya huduma ndogo za fedha kwa upande wa vyama hivyo katika usimamizi wao.

Alisema pamoja na hilo lakini pia kanuni ya mwaka 2019 ya kupitia sherua ya huduma ndogo za fedha waliamua elimu hiyo ili watu waweze kufahamu nini kinachpaswa kukwenye sheria hiyo na nini kinachoppasa kutekelezwa kwenye miongozo mbalimbali ya chama.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Hills View wilayani Korogwe mkoani Tanga ambapo alisema lazima uwekezaji huo wa mikopo uwe kwa wanachama na hiyo ni kwa mujibu wa baraza la ulimwengu linalosimamia vyama vya ushirika na akiba kwamba linaelekeza kwamba mikopo ielekezwe kupitia viwango vya kufanya uchambuzi.

“Hivyo ni muhimu kuhakikisha kwamba vyama vinawekeza nguvu kubwa kwenye kutoa mikopo kwa wanatoa mikopo kwa wanachama kwa lengo la kuwawezesha “Alisema

“Lakini tunapokwenda kutekeleza sheria ya huduma ndogo ya fedha kila Saccos imeelekezwa kuwa na sera ya uwekezaji na hiyo ni muhimu kutokana na viatarishi vilivyopo kwenye sekta ya huduma ndogo za kifedha hususani kwenye vyama vya Sacoss.

Alisema kwa hiyo kuwa na sera hiyo itaiwezesha kuweza kuona maeneo gani ambayo ni hatarishi ili ule uwekezaji unaokwenda kufanyika kupitia vyama uwe na tija kwa manufaa ya chama,wanachama na Taifa kwa ujumla.

“Lakini pia vyama vinaaswa kuelekeza na kwamba vihakikishe vinaanda hiyo sera ili kuepukana na viatarishi vya uwekezaji ambavyo vinaweza kuwa vikwazo katika kupata mafanikio”Alisema

Akizungumzia suala la viatarishi ambapo alisema maeneo mengine sacos zinaweza kuwekeza kwenye mabenki au taasisi za kufedha lakini kabla hazijafanya uwekezaji lazima uhakiki wa kutosha kwamba maeneo gani hatari ambayo unaweza kupeleka fedha zisirudi na kuleta matokeo yanayotarajiwa.

“Kuna mabenki mengii yamekuwa yakifungwa hivyo kama vyama vyetu vingekuwa wamepeleka fedha huku mwisho wa siku zingekuwa zimepotea ni vema sacos na viongozi wa bodi kupitia mikutano yao mikuu wakaona namna ya bora ya kufanya uwekezaji kupitia taarifa za makampuni mbalimbali yanayochapisha taarifa zao kwenye vyombo vya habari” Alisema

Aidha alisema kwamba lazima vyama vimeelezwa uwekezaji wa fedha zake uwe asilimia 70 hadi 80 kwenye mikopo hivyo hawatarajii vyama kuweka fedha nyingi zinazokwenda kuwekezwa nje kwa sababu kuwa imara vyama vya akiba na mikopo ni kutoa fedha kwa wanachama kwa kufanya hivyo fedha zikiwekewa huko zitakuwa salama zaidi kuliko maeneo mengine.

Awali akizungumza wakati mafunzo hayo Mrajisi Msaidizi anayesimamia vyama vya ushirika wa kifedha Josephat Kisamalala alisema tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania imekasimishwa majukumu yake ya usimamizi wa vyama vya Sacoss kutoka benki kuu ya Tanzania kwa mujibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka namba 10 ya mwaka 2018.

Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria hiyo ya benki kuu ya Tanzania imeelekezwa kukasimisha majukumu yake kwa mamlaka ambazo zinaweza kuwasaidia kusimamia taasisi za kifedha na tayari benki hiyo imeshakamisha majukumu yake kwa tume ya maendeleo ya ushirika na baada ya tume kukasimishwa iliona ni bora ianze kujipanga.

Alisema baada ya kukasimishwa waliona Mrasjis wa vyama vya ushirika Tanzania aliunda kikosi kazi kwa kushirikiana na wadau wa vyama vya ushirika kutengeneza nyaraka za mfano ambazo zitasaidia sacos kuweza kuomba leseni.

Aidha aliongeza kwamba kwa mujibu wa sheria hiyo hakuna taasisi inayoweza kutoa huduma ndogo za kifedha bila kuwa na leseni ya usimamizi baada ya kukasimishwa na jukumu wanalo lifanya ni kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wote wa sacos nchi nzima ili waweze kutekeleza vema sheria hiyo.

Naye kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Tanga Jackline Senzige alisema kwamba kwa sasa kwenye sheria ya vyama vya ushirika kuna vyama vya akiba na mikopo vinavyopitia kwenye michakato mbalimbali.

Alisema kwamba wanapoihuisha sheria ya huduma ndogo ya fedha ya mwaka 2018 ili iweze kutekeleza kwa vyama vya ushirika kwa mkoa wa Tanga wanatoa mafunzo kwa vyama hivyo lengo kupitishana kwenye sheria zote ili waweze kuzielewa kwa ajili ya utekelezaji.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: