Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Himid Njovu akizungumza na wanahabari leo 
Mstahiki meya Alex Kimbe katikati akizungumza na wanahabari 


SAKATA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kutaka kumng'oa Mstahiki meya Alex Kinbe (CHADEMA) lazidi kumwendea vibaya Kimbe baada ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Himid Njovu kuibuka na kumtaka meya huyo kujibu tuhuma zake vinginevyo kura zitamuondoa.

Kuwa anachokifanya meya Kimbe kwa sasa ni kujaribu kutafuta kichawi wa tuhuma zake jambo ambalo anazidi kupoteza muda wa siku tano aliopewa kujibu tuhuma hizo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Iringa ,Njovu alisema kuwa madiwani waliotoa tuhuma hizo kwa kujiorodheza ni pamoja na madiwani wa chama chake cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na wale wa chama cha mapinduzi (CCM)  hivyo hoja yake ya kutaka kupewa majina ya madiwani waliosaini azmio hilo hawezi kupewa jibu sasa kwani si wakati wake kupewa ushahidi.

Kuwa yeye anatakiwa kujibu hoja za tuhuma zake zote anazotuhumiwa na madiwani ikiwemo tuhuma ya matumizi mabaya ya gari ,Rushwa ya ngono na nyingine kama alivyoorodheshewa kwenye barua aliyopewa.

Aidha Njovu alisema anashangazwa na madai yanaoandikwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa meya anataka kununuliwa kwa shilingi milioni 200 na kutaja watu wanaotaka kumnunua na kuituhumu ofisi yake kuwa anapoteza muda maana hana hakika kwa muda uliobaki kama kuna  chama kinataka kutumia fedha hizo kwa sasa.

"Ninachokiona ni kujaribu kutafuta huruma na kutafuta mchawi katika tuhuma zake maana yeye ametunukiwa na madiwani anapaswa kuwajibu "

Alisema  kuwa madiwani waliomtuhumu meya wametimiza vigezo vyote vya kufikisha tuhuma zao .

Hata hivyo alisema tume itakayoundwa na mkuu wa mkoa kuchunguza tuhuma hizo ndipo ambapo ushahidi wa pande zote utakapohitajika ila sio sasa kuweka wazi majina ya wanaomtuhumu .

Aidha alisema kwa upande wake kama mkurugenzi hawezi kujibu tuhuma yoyote alitotuhumiwa meya kwani kwa kufanya hivyo ni kumsaidia majibu maana aliyetuhumiwa ni meya na sio mkurugenzi .

Alisema kuwa kwa sasa ataendelea na nafasi yake ya umeya hadi pale mkutano utakapoitwishwa kwa ajili ya kufanya maamuzi  kwa njia ya kupiga kura za siri na wakipiga kura zikitimia kura za kumtoa atatoka na kama hazitatimia basi atabaki.

Pia alisema kuwa tuhuma za meya ikiwemo ya rushwa ya ngono hazijaingilia uhuru wa mahakama maana zimegusa kanuni za kimaadili ya mtumishi wa umma ambayo kila mmoja anapaswa kuzitekeleza.

Alisema kuwa kanuni ambazo madiwani wamezitumia kumkataa meya wao ni kanuni ambazo zilipishitwa kwenye baraza la madiwani kwa madiwani wote kuzifuata .

 Hivyo alisema kanuni liyotungwa na kupitishwa na wao wenyewe madiwani hivyo meya anapaswa kutekeleza badala ya kukwepa kuitekeleza.

Aidha alisema kura zinazoweza kumuondoa meya madarakani pindi kikao kitakapoitishwa ni kura theruthi mbili ya madiwani wote katika Halmashauri hiyo .

Alisema kwa sasa baada ya madiwani kadhaa wa CHADEMA kujiuzulu CCM ina madiwani 14 na CHADEMA wana madiwani 12.

Kwa upande wake Meya Kimbe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea barua hiyo alisema kabla ya kujibu tuhuma hizo anataka mkurugenzi kumpa orodha ya madiwani 19 waliojiorodhesha kumkataa apate kuwajua maana madiwani wake wa CHADEMA wote wamekata kushiriki njema hiyo ya kumng'oa .

Aidha alisema kama mchakato wa kumng'oa utalazimishwa na serikali basi atakwenda mahakamani kupinga mchakato huo .

Toka meya Kimbe ameandikiwa barua  hiyo February 27 mwaja huu tayari siku tano zimepita .
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: