MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Manyara imesababisha shughuli mbalimbali za kijamii kusimama katika kata ya Kisangaji wilayani Babati huku wanafunzi wakishindwa kuvuka kwenda shule.Mwandishi John Walter anaripoti kutoka Manayara 

Aisha Binde mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Shaurimoyo, anasema hali hiyo ya mafuriko inawalazimu wazazi kuwapeleka shule na wakati mwingine hukuta mwalimu kashamaliza kipindi.

 Hali hiyo imepelekea mahudhurio ya wanafunzi katika shule hiyo kushuka,utoro na hata vwengine kukatisha kabisa masomo.

 Mwalimu wa Taaluma katika shule ya Msingi ShauriMoyo Said Mbwambo, anasema hali ya Taaluma katika shule hiyo ni mbaya kutokana na kukosekana miundo mbinu rafiki ya bara bara za kuwawezesha wanafunzi kufika shuleni kutokana na mafuriko.

 Wananchi wa kijiji cha Kisangaji wanaziomba mamlaka husika zishughulikie changamoto hiyo ili waweze kufanya shughuli zao za kila siku.

 Diwani wa kata ya Kisangaji Adam Ipingika anasema serikali tayari imeshatambua maeneo yenye changamoto ya daraja na kwamba zaidi ya shilingi Milioni 400 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja na vivuko.

 Aidha diwani huyo amesema zaidi ya kaya 100 zimekosa makazi kutokana na mvua kubwa kusababisha mafuriko katika maeneo yao na kueleza kuwa serikali ya kijiji inaendelea kutafuta hifadhi kwa ajili ya wahanga hao.

 Hata hivyo mvua za Msimu huu hapa nchi zimeathiri maeneo mengi ya mkoa wa Manyara.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: