Wednesday, 11 March 2020

Mkurugenzi Yes -Tz ,Elimu ya mahuasiano inamjenga mtoto wa kike


Na Esther Macha, Mbeya
MKURUGENZI wa shirika la Youth Education Through Sports Tanzania (YES -TZ), Keneth Simbaya amesema kuwa elimu ya mahusiano inamjenga mtoto wa kike kukabiliana na vishawishi vyovyote kutoka kwa mwanaume pindi anapokuwa kwenye masomo au kwenye  shughuli nyingine.
Amesema kuwa siku ya wanawake inapaswa kubebwa ajenda ya kuwafunda, mabinti .
Aidha Simbaya alisema moja ya mikakati ya Shirika la (YES TZ) ni kuhakikisha watoto hususani mabinti wanatimiza ndoto zao kwa kuhakikisha wanakuwa na afya njema, wanapata elimu ya demokrasia na utawala bora sambamba na kujifunza ujasiriamali.
Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi huyo wakati wa wa sherehe za maadhimisho ya  siku ya wanawake duniani, ambapo shirika hilo liliwakutanisha wanafunzi wa shule za sekondari, mabinti  waliokabiliana na vikwazo mbalimbali na walimu  kwa lengo la kutafakari  siku hiyo muhimu.
Mmoja wa walimu walioshiriki kilele cha sikukuu  hiyo, Joyce Mwakalinga kutoka shule ya sekondari Samora,aliwashauri wazazi kutowapendelea watoto wa kiume katika mahitaji badala yake waweke usawa.
Mratibu wa Shirika la Youth Education Through Sports Tanzania (YES- TZ), Navina Justine, alidai sikukuu ya wanawake duniani inatoa nafasi kwao kutafakari juhudi zilizofanywa na wanawake walioanzisha siku hiyo maalum, kujadiliana kwa pamoja vikwazo vinavyowakabili na kutambua fursa zilizopo kwenye jamii ili kujikwamua na umasikini.
 Mwisho.


No comments:

Post a comment