Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Chama cha  Skauti Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na
kupambana na Rushwa nchini ,TAKUKURU kimeandaa mpango kabambe wa kutoa
elimu ya rushwa  katika shule  kwa ngazi mbalimbali hapa nchini.

Mpango Kabambe wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa mapambano dhidi ya rushwa kwa kutumia vijana wa skauti unazinduliwa Leo katika chuo kikuu cha Dodoma na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mskauti mkuu Tanzania Mwamtumu Mahiza wakati akizungumza na Wanahabari alisema kuwa wameamua kutoa elimu kwa shule za msingi
sekondari na vyuo vikuu juu ya  madhara ya rushwa ikiwa ni pamoja na rushwa ya ngono  huku akiwaasa
vijana kuwa na  uzalendo, uchungu na nchi yao .
Alisema kuwa viongozi wa skauti walianza mkakati wa kufahamu vitu
ambavyo vijana shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu vinawasumbua
na kugundua ni rushwa hususani ya ngono.

Alisema maskauti vijana kuanzia miaka 7 hadi 26 rushwa inawaathiri na
kupelekea  mimba za utotoni pamoja na maambukizi hivyo watakua wanatoa
elimu ya Mara moja kwa wiki kila shule za msingi, sekondari, na vyuo.
"Rushwa iwe sumu, adui tunakosa haki kwa sababu ya rushwa kupoteza
maendelea ya Taifa, inakosesha amani na upendo katika nchi yetu ya
Tanzania
" Pakiwa na rushwa kwenye nchi huwezi ukawa na taasisi imara, huwezi
kuwa na amani huwezi kutenda haki kwa sababu kila kitu kitakuwa
kinaongozwa na rushwa". Alisema Mwantumu.
Mwantumu amefafanua kuwa  zipo takribani shule 17,520 zenye takribani
wanafunzi milioni 8 kila mwanafunzi akiweza kuielewa rushwa ni nini na
akiweza kuzungumza na watu wanne tu watakuwa wamegusa watanzania
million 32 ambapo janga la rushwa litapungua kwa asilimia kubwa.
Pia Mwantumu amesema kuwa kwa upande wa vijana hao wa shule za msingi,
sekondari na vyuo vikuu ili waweze kuwa wanaskauti bora ni pamoja na
kujiepushwa na rushwa, kuipenda nchi yao, kujitoa kwa ajili ya nchi,
kuheshimu mamlaka na kumtii mwenyezi mungu.
"vijana hii ndio nchi yetu hakuna nchi yoyote ambayo haina changamoto
hivyo ni vyema kutenda matendo yaliyo na haki na usahihi katika Skauti.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema Takukuru mkoani Dodoma inaendelea na tafiti juu ya kiwango cha rushwa ya ngono Dodoma na makubaliano na skauti itakuwa mwarobaini wa mapambano ya rushwa kwani vijana Wa skauti ni mabalozi wazuri dhidi ya mapambano ya rushwa shuleni na taifa kwa ujumla.

   kauli mbiu katika uzinduzi wa mpango huo ni Kupambana na rushwa ni jukumu langu .

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: