Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa ya Asas Ahmed Asas akizungumza na waandishi habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wadau wa afya walipokuwa wakijadili kuhusu kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
 
Serikali ya wilaya ya Iringa imeipongeza kampuni ya Asas kwa mikakati ambayo wanayo katika kuhakikisha wanajilinda na maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimekuwa tishio kwa maisha ya binadamu.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema mkakati ambao wanaoutekeleza kwa kujilinda na virusi vya Corona kwa wafanyakazi wake.

"Nimeona wametenga chumba maalumu kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wake na tayari ameshatoa mafunzo kwa wafanyakazi watatu kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza kwa wale ndio watakaohisiwa wanamaambukizi ya virusi vya Corona"alisema kasesela

Kasesela alisema kuwa kampuni ya Asas imefanikiwa kutoa elimu ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia vyombo vya habari na makundi mbalimbali hivyo ni mfano wa kuigwa.

Aliitaka kampuni ya Asas kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa wananchi wote wa wilaya ya Iringa ili kuokoa maisha yao katika kipindi hiki kigumu

Kwa upande wake mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa ya Asas Ahmed Asas alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa waandishi wa habari,wafanyakazi wa kampuni ya Asas na taasisi binafsi kwa lengo la kuepuka kuambukizwa virusi vya corona.

Ahmed alisema kuwa kwenye kampuni ya Asas wamefanikiwa na kuwa na chumba maalumu kwa ajiri ya wafanyakazi watao kuwa na dalili za maambukizi ya virusi vya corona na wameganikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi kwa lengo la kuwa msaada kwa wafanyakazi wengine. 

"Sisi tupo tayari kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona sehemu yeyeyo ile kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Iringa kama ambavyo yumeanza na mkuu wa mkoa wa Iringa Richard kasesela" alisema Ahmed
Share To:

Post A Comment: