Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mbarali 


Na Esther Macha, Mbarali


KAMATI ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mbarali ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya  , Reuben Mfune imeridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwa ajili ya kuwapokea wahisiwa pamoja na wagonjwa wa Corona (COVID 19) watakaothibithishwa na wizara ya Afya.

Hayo yamesemwa leo wakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea maandalizi ya jengo hilo ambalo lipo kitongoji cha mpunga Relini ambako inajengwa hospitali mpya ya wilaya.

 Hata hivyo Mfune alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuendelea kufanya maboresho madogo magogo kama usafi wa mazingira ili eneo hilo liendelee kuwa katika hali ya usafi.

“Katibu Tawala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, muwe mnapita mara kwa mara kwa ajili ya kujiridhisha na kuendelea kuboresha mazingira haya hasa suala la usafi, vilevile muendelee kuwasimamia mafundi ili kazi ndogondogo zinazoendelea ziweze kukamilika kabisa na elimu ya kujikinga na ugonjwa huu iendelee kutolewa kwa wananchi kwa sehemu zote muhimu”


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: