Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kukabiliana na Wizi wa Magari,Jeshi la Polisi limeanzisha Operesheni maalum ambapo hadi sasa jumla ya Magari  ya wizi 130 ,Pikipiki 193 na vipuli 753 na watuhumiwa 128 wameshakamatwa
Hayo yamesemwa leo Machi 28,2020 jijini D  odoma na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai hapa nchini [DCI]   Kamishna wa Polisi ,Robert Boaz  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.
Kamishna Boaz amesema  uchunguzi unaendelea kufanyika ili kuweza kubaini wahalifu wa Makosa mbalimbali.
“Kipindi hiki tumeshuhudia dalili za ongezeko la makosa ya wizi wa magari na Matukio haya mara nyingi yamekuwa yakitokea usiku watu wakiwa wameegesha magari hayo na wezi wamebuni mbinu mbalimbali za kufungua na kuwasha magari hivyo jeshi la polisi limeanzisha operesheni Maalum ambapo hadi sasa jumla ya Magari ya Wizi 130 yameshakamatwa na uchunguzi unaendelea”amesema
Aidha Kamishna Boaz  amebainisha  kuwa katika kipindi cha  Miezi miwili ya kwanza kuanzia Januari hadi Februari Mwaka huu  hali ya uhalifu imezidi kupungua kutoka Matukio makubwa ya uhalifu  elfu tisa mia tano na sabini na mbili[9572] hadi Makosa   elfu tisa mia mbili sitini na tatu[9263 ] ambapo ni sawa na upungufu wa matukio mia tatu na tisa[309] ikiwa ni sawa na  asilimia  3.2%.
Kuhusu Makosa ya Usalama barabarani Kamishna Boaz amesema yamepungua kutoka 533 hadi makosa 425 sawa na upungufu wa makosa 108 sawa na asilimia 20.3% .
Pia  Kamishna Boaz ametoa tahadhari kwa wananchi kufuata taratibu pindi wanaponunua magari makuukuu ikiwa ni pamoja na kwenda kulikagua polisi hali itakayosaidia kujiepusha ununuzi wa magari ya wizi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: