Friday, 6 March 2020

DC MWERA AHAMASISHA WANANCHI WA BUSEGA KUJITOKEZA KWA KUMPOKEA MAKAMU WA RAIS


MKUU  wa Wilaya ya Busega,
Mhe.Tano Mwera (pichani)amewaomba wananchi kufika kwa wingi katika Viwanja vya Benki mpya ya NMB Busega hapo leo tarehe 06 March 2020 Kuanzia saa moja asubuhi kwa ajiri ya kumlaki na kumsikiza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.

Mh. Samia Suluhu  atakuwa na ziara ya siku 3 Mkoani Simiyu.

Mkuu huyo amesema akiwa Busega Mhe Samia Suluhu Hassan atafungua tawi la Benki ya NMB na kuongea na wananchi wa Busega.

"Nahamasisha wananchi wa Busega kuhudhuria kwa wingi kumsikiliza  Mama yetu Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Kesho Machi 6, tujitokeze mapema sana  kuanzia saa moja asubuhi kwa ajili ya kumlaki na kumsikiliza kwani ataanzia hapa ziara yake ndani ya Mkoa wetu ni fursa ya kipekee" alisema DC Mh.Tano Mwera.

Aidha, Mkuu huyo amesema hali ya ulinzi na Usalama ya Busega ni shwari na maandalizi ya kumpokea yamekamilika kwa asilimia 95.

Tarehe 08/03/20 Mh.Makamu wa Rais atahitimisha Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa inafanyika Mkoani Simiyu Chini ya Kauli Mbiu;  "Kizazi Cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadae" . Wote mnakaribishwa.

Mwisho.

No comments:

Post a comment