Wanawake wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa wa saratani wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocen Road iliyopo jijini Dar es saaalm.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya wanawake wengine wa Chuo hicho Mkuu wa Idara ya jinsia Dkt. Sarah Nwakyambiki amesema msaada waliotoaa ni sehemu ya jukumu la Chuo katika kuijali jamii.

“Hiki tunachokabidhi ni sehemu ya jukumu la Chuo katika kuijali Jamii, ambapo hii leo katika kuelekea na kuadhimisha siku ya wanawake tumekabidhi vifaa tiba, Kanga, Sabuni, taulo za kujihifadhi na dawa za meno,” alisema Dkt. Sarah.

Akizungumzia nafasi ya Chuo hicho katika kujitoa kwenye Jamii Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila amesema pamoja na Chuo kuwa na jukumu la kutoa mafunzo ya kitaaluma, uongozi na maadili, lakini pia ina jukumu la kutoa huduma za kijamii kama ambavyo wanawake wa Chuo hicho wamekabidhi msaada kwa wahitaji wa Taasisi ya Ocean Road.

“Wanawake wa chuo leo wametoa msaada kwa wagonjwa wa Taasisi ya  ya Ocean Road, pamoja na Wanawake kupima afya zao, ikiwa ni pamoja  na saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya matiti, amesema Prof. Mwakalila.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano,
Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,
06.03.2020
Share To:

msumbanews

Post A Comment: