Tuesday, 24 March 2020

CCM MKOA WA MBEYA KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI JUU YA CORONA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya, Mchungaji Jakob Mwakasole  akizingumza na waandishi wa habari

PNa Esther Macha, Mbeya

CHAMA cha mapinduzi Mkoa wa Mbeya kimesema kuwa kimepokea kwa mikono miwili kutekeleza agizo la serikali la kuelimisha wananchi juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Hayo yasemwa jana Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya , Jakob Mwakasole wakati akizungumza na waandishi wa habari jinsi walivyopokea maagizo ya wizara ya afya ya  kujikinga na  homa ya Corona.

Mwakasole alisema chama hicho kimepokea maelekezo yote na kimeendelea kutekeleza na kimewaagiza viongozi wa matawi kuelimisha wananchi waliopo vijiji kujikinga na ugonjwa huo wa Corona ambao hivi sasa tatizo kubwa kwa dunia.

Aidha Mwakasole alisema wanaendelea kuwasiliana na serikali ili wataalamu waweze kufika vijijini kutoa elimu kwa wananchi.

“Tunaomba wananchi waendelee kuomba kwa mungu ili ugonjwa huu uishe na pia wananchi wafuate maelekezo ya wataalam ambayo yanatolewa katika kujikinga na ugonjwa huu tusipofuata maelekezo ya wataalamu tutapotea hivyo tusipuuze”alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema kuhusu uvaaji wa kinga alisema endapo vitavaliwa vibaya inaweza kuhatarisha maisha kwa kupata maradhi mengine kutokana na uvaaji mbaya usiozingatia taratibu za wataalam wa afya kwani ugonjwa huu bado ni mgeni .


No comments:

Post a Comment