Mchungaji wa kanisa la Pentecoste Arusha mwalimu Onesmo Nnko wa Kwanza kulia akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro mashine ya kusafishia njia ya hewa kwa watoto wachanga Kama ishara ya kukabidhi misaada yote walioitoa kwa kituo Cha Afya USA River 

Na Woinde Shizza , MsumbaTv

Kanisa la Pentecoste Ngulelo linaloongozwa na Mwalimu Onesmo Nnko limekabidhi vifaa vya afya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya kanisa na Serikali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo ambavyo vimetolewa kutokona na sadaka za waumini wa kanisa la Pentecoste Arusha Jana , kiongozi wa kanisa hilo mwalimu Onesmo Nnko amesema wao kama kanisa wana kila sababu ya kuungana na serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya ili kutengeneza jamii bora 

Alisema kuwa kanisa lao limekuwa likitoa misaada mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu ,misaada kwa watu mbalimbali na kipindi hichi wameamua kutoa katika sekta ya afya na wameanza na kituo Cha Afya Cha Usa river  na wanampango wakiendelea kutoa msaada katika vituo vingine vya afya vilivyopo katika mkoa huu.

"Nimeguswa kutoa katika jamii na ndio maana nikawaamasisha waumini watoe ili kutimiza maono nilionyeshwa na mungu,na tukumbuke kwamba ata katika mistari ya biblia imeandikwa nibora kutoa kuliko kupokea ,hivyo napenda kiwasihi wananchi wapende kutoa kuliko kupokea ,tusitoe kwa vile tunacho bali tutoe ili tukapokee zaidi,na jinsi tunavyotoa ndivyo mungu anatukumbuka katika mahitaji yetu "alisema Onesmo

Aliwataka viongozi wengine wa dini  kuendelea kushirikiana na serikali katika  maswala mbalimbali kwani serikali na kanisa ni mikono miwili ya kusaidia jamii.


Akipokea misaada hiyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro amesema kupatikana kwa vifaa hivyo kutasaidia kuimarisha huduma pamoja na kuondoa changamoto ya uhaba wa vifaa vya kutolea huduma 

"Kweli vifaa hivi vitatusaidia kwani tulikuwa na uhaba wa baadhi ya vitu katika kituo hichi Cha Afya  ,hivyo hivi vilivyotolewa vitatusaidia sana napenda nikushukuru mwalimu Onesmo pamoja na waumini wako kwa kuamua kujitoa  kwa ajili ya kutununulia baadhi ya  vifaa tiba kwa ajili ya kituo chetu Cha Afya niwaombe viongozi wengine wa dini muige mfano huu"alibainisha Muro

Akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za afya katika Halmashauri, mganga mkuu wa wilaya Dkt. Maneno focus amesema kwa sasa huduma za afya zinazidi kuimarika na wameamua misaada hiyo itolewa katika kituo cha afya cha usa river ambacho Mhe Rais Magufuli alitoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi ambao ulishakamilika na kituo kinatoa huduma za kisasa 


Mmoja ya mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la  Edna  Ulomi  alishukuru serikali kwa kiwasogezea huduma na kubainisha kuwa awali walikuwa wakipata tabu kwenda kupata huduma katika hospital ya wilaya ya patandi,aliongeza kuwa wauguzi wamekuwa wakiwapatia huduma Bora na nzuri kuliko vituo vingine .

Vifaa vilivyotolewa na kanisa Hilo la Pentecoste Arusha ni pamoja na mashine ya kusafishia njia ya hewa kwa watoto wa changa (sunction machine),vitanda 6 ,mashika 100,deliver set 3,matress for neonatial unit,oxgen cycliner eflow meter 1, Mercury Bp machine 3, hospital screen 1,Bigstetcher 1,pamoja na Exmination bed 2.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: