Na.Vero Ignatus,Arusha

Jamii imetakiwa kuondoka na na dhana potofu ya kumkeketa mtoto wa kike na kumuondolea hadhi na utu wake kama Mungu alivyomuumba badala yake wabadilike na kukemea kitendo hicho kwani ni ukiukaji wa haki za kibinadamu

Ukeketaji unawaathiri wasichana na wanawake kwa asilimia kubwa pia kitendo hicho kinadhoofisha uchumi pamoja na nguvu kazi, unaathiri afya ya mwili na akili za kwa wanawake wanaokeketwa hivyo jamii inapaswa kuungana ili kupinga kitendo hicho

Hayo yamesemwa na Muwakilishi wa dini ya Wahabai mkoani Arusha John Msabi kwamba mtu yeyote aliyepo karibia na jamii awe muhamasishaji wa kupinga mila hizo mbaya na potefu zinazomkosesha ujasiri mtoto wa kike na mwanamke

Msabi amesema mara nyingi watoto wa kike na wanawake hufanyiwa tunyanyasaji huo kwa lazima na kwa maumivu makubwa, amekemea baadhi ya makabili yanayoamini kuwa mwanamke asiyetahiriwa hawezi kuolewa jambo ambalo halina ukweli wowote
  
 Ikumbukwe kuwa unapomkeketa mtoto wa kike unamsababishia maumivu makali,kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua  kwani  kovu lililopo  halitanuki hivyo humsababishia maumivu makali  na hata wakati mwingine hupelekea kupoteza Maisha yake pamoja na mtoto

Hivyo basi Kila mwanajamiii anapaswa kushiriki kampeni kuhamasisha na kupiga vita suala la ukeketaji kwa watoto wa kike na wanawake kwa ujumla

Ameitaka jamii kutambua kuwa mtoto wa kike ni tunu hivyo unapomuelimisha mwanamke umeielimisha jamii nzima kwasababu muda mwingi ndiyo wanakuwa na watoto familia kwa asilimia kubwa kwa muda mrefu

‘’Kama wewe ni mwalimu ,mchungaji ,shekhe kiongozi wa serikali kuanzia ngazi zi za mtaa hadi Taifa siasasa wakati unaendelea na taratibu za kufanya majukumu yako ya kila siku hakikisha umegusia suala hili la kupinga ukeketaji kwa Watoto wakike na wanawake’’

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha  Yasmini Bachu amewataka mamgariba ambao bado wanaendeleza tabia hiyo kuacha mara moja sambamba na kuwaonya waache wanawakeketa watoto wachanga 

'Bachu amesema kuwa baada ya kuona serikali inakemea kitendo cha ukeketaji kwa nguvu zote,mangariba wamebuni mbinu ya kuwakeketa watoto wachanga kuanzia mwezi mmoja hadi miwili jambo ambalo ni hatari sana 

‘'Tuwalaani mangariba wote am,bao wanafanya kazi hiyo ya kuwakeketa Watoto wachanga jambo hili ni baya sana na sisi hatutanyamaza bali tutapaza sauti kukemea suala hili’alisema

Alisema ndoa changa zinakuwa na migongano na kuvunjika kutokana,kuwa na migogoro mingi isiyokwisha ila sehemu kubwa chanzo chake unakuta mwanamke amekeketwa

Amesema kuwa ukeketaji husababisha matatizo ya kiungo pamoja na yale ya kiakili kwa mwanamke katika kipindi chote cha Maisha yake kilichosalia kwasababu huathirika kisaikolojia siku zote

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO) limesema kuwa ukeketaji unaathiri wasichana na wanawake na gharama ya matibabu ni dola bilioni 1.4 kwa mwaka kimataifa iwapo mahitaji yote ya kiafya yatashughulikiwa.

 Siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji hufanyika kila mwaka februari sita 

MWISHO


Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: