Saturday, 15 February 2020

SWAHILI ENCOUNTERS 'NI NOMA SANA' WAPIGA SHOO MATATA SAUTI ZA BUSARANA ANDREW CHALE, ZANZIBAR

WASANII muunganiko kutoka nchi Sita, United  Kingdom  (UK), Morocco,  Ghana, Algeria,Tanzania  na visiwani Zanzibar  wamefanya onyesho moja matata lililokonga nyoyo mashabiki wa muziki usiku wa pili wa tamasha la Sauti za Busara Februari 14..

Onyesho hilo la pamoja wasanii hao kwa kila mmoja alionyesha uwezo wa sanaa yake

Kupiga ala za muziki, kuimba na kucheza ambapo kila mmoja aliweza kuonyesha kitu cha tofauti katika  onyesho lao la hilo.

Wasanii Ester  Subi Zawose na Pendo Ukwe Zawose (Tanzania Bara) waliweza kuonyesha ngoma ya Wagogo katika muunganiko wa onyesho hilo.

Msanii Siti Amina (Zanzibar ) nae aliweza kuonyesha uwezo wake jukwaani ikiwemo ule wa kuimba na kucheza.

Munganijo wa vyombo uliojaa ustadi na ubora wa hali ya juu ulitosha kutoa radha halisi ya muziki wa Afrika ambao umekuwa ni wenye kuvutia jamii nyingi.

Wasanii hao pia waliweza kuimba wimbo  'Sawa sawa'  ambao unaendana na ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka huu wa tamasha wa kupinga na kukemea unyanyasaji wa kujinsia.

No comments:

Post a comment