.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akifungua kikao cha tathimini  ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya mkoa ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo  Asia Abdallah na kushoto ni katibu tawala mkoa wa Iringa Happines Seneda 
Mdau wa Lishe mkoa wa Iringa Lediana Mng'ong'o akichangia katika kikao hicho .

.....................
Mkuu wa mkoa wa Iringa  Ally Hapi amewataka viongozi wa Halmashauri na wadau kushirikiana kupunguza  kasi ya  udumavu  kwa  watoto  wenye  umri wa miaka  chini ya 5 kutoka  asilimia  47 kwa  sasa   hadi  kufikia  angalau  asilimia 35 ifikapo  mwaka 2021.

 Hapi ametoa  agizo   hilo leo  wakati akifungua  kikao  cha  tathimini ya  utekelezaji wa  mkabata  wa  lishe  kwa  kipindi  cha julai  hadi Disemba 2019 ,mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Ally  Hapi  alisema  kuwa iwapo  mikakati  ya  kupunguza kasi ya udumavu ambayo  mkoa  umeweka  ikatekelezwa  kwa  wakati  na kwa  uhakika   upo  uwezekano  mkubwa wa asilimia za  udumavu  zikapungua  zaidi.

Pia alitaka Halmashauri  Halmashauri  kutenga   fedha  katika  mipango yake ya  maendeleo  angalau  shilingi  1000 kwa  kila mtoto  chini ya  miaka mitano  na kuhakikisha   fedha   zinazotolewa  kutekeleza  afua za  lishe .

Alisema   kuwa  tatizo la  lishe  katika  jamii ya  mkoa  wa  Iringa bado ni  kubwa   na kutokana na hali    hiyo  serikali  imeendelea   na  jitihada  mbali mbali za kutafuta  tatizo  la lishe  mkoa ikiwa ni  pamoja na kusimamia uwajibikaji wa  afua za  lishe .

"  Ikumbukwe  kuwa  mwaka 2017  mkoa  ulisaini  mkataba  wa  utekelezaji wa masuala ya  lishe  na  mwaka 2019  mikataba  hii imeshushwa  hadi  ngazi ya  kata  na  vijiji  lengo likiwa ni kuhakikisha  utekelezaji ,usiamizi na uwajibikaji wa afua  mbali mbali za  lishe  unaratibiwa  kuanzia  ngazi za vijiji  na mkitaa na  juhudi  za  utekelezaji wa mikataba  hiyo zilete  matokeo katika kupunguza  tatizo la utapiamlo hasa udumavu katika  mkoa wa  Iringa "  alisema Hapi

Mkuu  huyo  alisema kuwa  udumavu kwa  mkoa  ni  asilimia  47  kiwango  ambacho ni kikubwa  kisichokubalika  ndani ya  mkoa  wa Iringa ambao ni mmoja  kati ya  mikoa ambayo inaongoza  kwa  uzalishaji wa mazao ya  chakula  nchini .

"  watoto  wa miezi 6 hadi  23  milo  inayotakiwa  kulingana na umri  wa wtoto ni  asilimia 23  tu ,watoto  wa miezi 6 hadi 23 wanaopewa mlo  wenye  mchanganyiko  wa vyakula tofauti  zikiwemo mboga mboga ,matunda na vyakula vyenye  jamii  ya  kunde  na nyama  ni  asilimia 25  tu "

Hivyo  alisema lazima  kuendelea  mkushirikiana  kupambana na hali mbaya ya  udumavu mkoani Iringa  kwani athari zinazosababishwa na lishe  duni ni nyingi  kama  kuchelewesha ukuaji  wa  ubongo  na  kupungua  uwezo wa  kujifunza,kushindwa  kuchangamkia fursa  ,uwezo  mdogo  wa  kupambanjua mambo  na  kufanya maamuzi .

Pia   kupungua kwa uzalishaji   kutokana na vifo  ,maradhi  na miili dhaifu ,kupungua  kinga  ya mwili  hivyo kuruhusu mashambulizi   ya magonjwa mbali mbali  pamloja na vifo vya watoto chini ya miaka  mitano na akina mama .

Alisema  kuwa baadhi ya sababu za  kuwepo  kwa tatizo  la utapiamlo katika mkoa  ni  pamoja na uelewa mdogo wa baadhi ya  wazazi  na  walezi  katika  maandalizi na matumizi sahihi ya chakula  kwa mfano kutokula na  kutokuwalisha watoto chakula mchanganyiko ,kutumia nafaka  zaidi kuandaa  vyakula  vya  watoto na sababu  nyingine  nyingi .

Katika  kuhakikisha mkoa unaendelea  kutekeleza malengo  iliyojiwekea  ya  kutokomeza  udumavu kwa  watoto  alitaka tathimini ya  utekelezaji  wa  mkakaba  wa lishe  ifanyike  kila kipindi cha robo mwaka katika halmashauri zote,kila Halmashauri  ihakikishe  inawatambua  wahudumu  wa afya  ya jamii (WAJA) waliopo katika  katika Halmashauri na  kuweka utaratibu  wa kuwapa vitendea kazi  na motisha ili  wawe na mazingira mazuri ya  utendaji kazi
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: