Thursday, 13 February 2020

Mweli aridhishwa na Ujenzi wa Mabweni, Jangwani SekondariNteghenjwa Hosseah  OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu (E) Gerald Mweli ameridhishwa na ujenzi wa mabweni mawili  katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani iliyopo Jijini Dar es salaam.

Mweli ameonyesha hali hiyo alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni hayo pamoja na miundombinu mingine inayoendelea kukarabatiwa katika shule hiyo.

Akizungumza katika ziara hiyo Mweli amesema mabweni  hayo mawili yatakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja hivyo wanafunzi 160 wakike watapata fursa ya kukaa katika mabweni hayo.

« Fedha hizi zimetolewa na Serikali maalum kwa ajili ya kuwasaidia na kuwajali watoto wa kike waweze kusoma kwa amani na wapate mazingira bora ya kujifunzia  katika kipindi chote cha masomo yao na kuwaondolea vikwazo vinavyoweza kuathiri kumaliza masomo yao kwa usalama « .

Aliongeza kuwa miundombinu ya shule hii ilikua imechakaa sana kwa sababu shule hii imejengwa mwaka 1928 na ni maalum kwa watoto wa kike pamoja n wale wenye mahitaji maalum wote wanasoma katika shule hii.

Halkadhalika Mweli alisema kuwa zaidi na ujenzi wa mabweni hayo Mhe. Rais John Pombe Magufuli alitoa shiling milioni 90 kwa ajili ya ukarabati wa miundombunu ya shule hiyo hivyo kwa kiasi  kikubwa zimesaidia kuifanya shule hiyo kuwa katoka hali nzuri.

Aidha alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika ndani ya mwezi mmoja na ahakikishe kuwa mabweni hayo yanapata vitanda vyote kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa katika shule hiyo kuyatumia.

Pia alikuwaambia Walimu wa shule hiyo kuwa waongeze juhudi katika kufundisha na kusimamia wanafunzi ili waweze kuondoa zero  na daraja la nne kabisa na kurudisha hadhi ya shule hiyo.

Mweli alimalizia kwa Kumuagiza Mkurugenzi wa Elimu Sekondari OR-TAMISEMI kuhakilisha analeta vitabu vya kutosha vya kujifunzia katola shule hiyo.

Mwisho.

No comments:

Post a comment